VETA Kihonda yatoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa zaidi ya 1500 | ZamotoHabari.

Chuo cha VETA Kihonda kimetoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa  zaidi ya 1500 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka huu lengo likiwa ni kupunguza ajali ambazo zinatokana na makosa ya kibinadamu.

Chuo cha VETA Kihonda  ni  Chuo ambacho kimebobea katika utoaji wa mafunzo ya udereva magari makubwa ambapo madereva wa magari makubwa wanatakiwa kupata mafunzo hayo hapo au vyuo vingine vilivyosajiliwa vikiwa na mafunzo hayo.

Mwalimu wa Udereva wa Magari Makubwa na Mabasi wa chuo cha VETA Kihonda William Munuo amesema kuwa madereva wengi wanajua kuendesha kwa kunyoosha katika barabara lakini kurudi nyuma ni tatizo ambapo wengi ndio wanasababisha ajali au kuangusha magari hayo na kuleta hasara kwa makampuni.

Munuo amesema mafunzo waliyoyaanza ni endelevu na kutaka madereva kuzingatia mafunzo hayo na kuyaishi katika kuendesha na hatimaye watakuwa madereva bora.

Munuo amesema mafunzo hayo yanafanya magari makubwa kuishi muda mrefu kutokana  na wakati mwingine yanapata ubovu kwa uendeshaji usiofuata utaratibu wa uendeshaji wa magari hayo.

Amesema kuwa licha ya kuwa na leseni madereva wa magari makubwa wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara kutokana na teknolojia za magari kubadilika kila mara.

Aidha amesema katika mafunzo ya vitendo baadhi wanajua kuendesha magari makubwa ya tela moja wengine ni wale wa tela mbili ambapo wanaweza wote kuendesha lakini wakiwekwa katika urudishaji gari hizo nyuma kuna changamoto hivyo changamoto hizo zinatatuliwa kwa kuwapa mafunzo.

"Hatuwezi kuwaacha watu waendelee kuendesha magari makubwa katika ujuzi wa mazoea lazima wapate mafunzo bora ya kuweza kuwa madereva bora na sio bora madereva"amesema Munuo.

Munuo ameyataka  makampuni kuhakikisha madereva wao wanapata mafunzo kila mara kwa faida ya kampuni hizo na kusaidia utunzaji wa magari hayo.
 Mkufuzi wa Magari Makubwa na Mabasi wa Chuo cha VETA Kihonda William Munuo akitoa maelezo wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa madereva wa kampuni ya MeTL jijini Dar es Salaam.
 Dereva akiwa katika mafunzo  ya vitendo ya kurudusha gari nyuma wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa madereva wa kampuni ya MeTL jijini Dar es Salaam.
 Dereva akienda kuweka kifaa kwa ajili ya usalama wakati wa kuunga tera
 Dereva akiangalia namna ya kuunga tera mara baada ya kupata mafunzo ya Nadharia
 Alama zilizotumika katika mafunzo ya vitendo ya kurudisha gari nyuma.
 Wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja na madereva wa magari makubwa katika kampuni ya MeTL.
Mkaguzi wa Kikosi cha Polisi wa  Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja madereva wa MeTL mara kufungua mafunzo.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini