MAADHIMISHO YA REDCROSS KITAIFA KUFANYIKA KIGOMA KESHO | ZamotoHabari.

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

TANZANIA Red Cross leo inaungana na Nchi 191 ulimwenguni katika maadhimisho ya siku ya Red Cross Duniani Mei 8, 2019 ambapo mwaka huu kitaifa yanafanyika Mkoani Kigoma katika Viwanja vya Mwanga community center.

Akiongea na waandishi wa habari ofisa habari wa Red cross Tanzania Godfrida Jola amesema kuwa Mgeni rasmi katika madhimisho hayo kesho anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce L. Ndalichako.

Alisema katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi atazindua bweni la wanafunzi katika shule ya Bitale Maalum iliyopo Mkoani humo iliyojengwa kwa michango ya wanachama na wafanyakazi wote ili kuwasaidiawatoto wenye ulemavu watimize ndoto zao.

Kauli Mbiu ya mwaka huu kimataifa ni " Upendo ". Ujumbe huu unamaanisha kwamba Red Cross inawafikia na kuwahudumia watu na jamii nyakati zote katika hali mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote kwa upendo.

Tanzania Red Cross Society inafanya kazi kwa bidii na kutoa huduma za Kibinadamu kwa kufuata Kanuni zake saba za Ubinadamu, Uadilifu, Kutopendelea, Uhuru, kujitolea, Umoja, na Kushirikiana Kimataifa, hii inaifanya jamii kuiamini na kukisaidia kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Jola alisema Red Cross imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma wakati wa maafa na dharura mbalimbali ikiwemo mafuriko, njaa, tetemeko, ajali mbalimbali za nchi kavu na majini, kushiriki juhudi za kuboresha afya ya jamii na kuhamasisha upatikanaji damu salama, huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi.

 Kwa miaka zaidi ya 20 imekuwa ikitoa huduma za kibinadamu kwa Wakimbizi, kwa sasa inatoa huduma za afya kwa zaidi ya wakimbizi 300,000 katika kambi za Nyarugusu (Wilaya ya Kasulu) na Mtendeli (Wilaya ya kakonko), pia inatoa huduma za kuwaunganganisha wana ndugu waliopoteana (Restoring Family Links).

Katika maadhimisho ya mwaka huu, kupitia matawi yake ya mikoa na wilaya Tanzania Red Cross imefanya shughuli za kijamii ikiwemo, kusafisha mazingira, kusaidia vikundi vilivyo katika mazingira hatarishi na kuhamasisha watu uchangiaji damu kwa hiari, michezo, kambi ya vijana, kupanda miti na mafunzo kuhusu huduma za afya ikiwemo huduma ya kwanza.

Alisema pia Wilaya ya Kasulu, kwa kushirikiana na Halmashauri husika TRCS imejenga maabara za kisasa katika vituo vya afya vitatu kikiwemo cha Rusesa katika kata ya Rusesa, Nyenge (Kurugongo)na hospitali ya Kimwanya iliyopo katika Kata ya Nyachenda.

Pia katika Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma TRCS kwa ushirikiano na Belgium Red Cross inaendelea kutekeleza mradi wa Maji na afya ya msingi kwa kuwasaidia wanachi kujenga vyoo vya kisasa na kujenga uzio katika vyanzo vya maji katika vijiji saba vya Buhigwe, Kavomo, Murela, Songambele, Bulimanyi, Nyamugali na Munyegera ambapo hadi sasa familia 200 wamesaidiwa vifaa na kujenga vyoo vya kisasa.

"Tunaiomba jamii kuendelea kutoa huduma za kijamii kwa kufuata maadili ya kibaadam na kyifikia jamii popote ilipo na kila wakati"alisema


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini