TFS YAWAPELEKA AMINI NA LINNA MSITU WA MAGAMBA KUFANYA YAO | ZamotoHabari.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umeamua kuwapeleka wasanii Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga katika hifadhi ya Msitu wa asili wa Magamba uliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya kurekodi nyimbo yao mpya ya Nimenasa.

Vivutio vilivyomo kwenye msitu huo ndio sababu pekee ya wasanii hao kwenda kurekodi sehemu ya video itakayokuwa kwenye wimbo huo wa Nimenasa ambapo TFS imeamua kutoa nafasi kwa wasanii hao kwa kutambua wanayo nafasi ya kutumia misiti ya asili kurekodi video yao.

Akizungumza na Michuzi Blog akiwa katika msitu wa Magamba Amini ndani ya msitu wa Magamba kuna kila kitu na pengine ambavyo havipatikani nchi nyingine yoyote zaidi ya Tanzania.

"Nimenasa ni wimbo wangu mpya ambao nimemshikirisha dada Linna.Ni moja ya wimbo matata sana, hivyo niliona nina kila sababu ya kufanya video yake katika eneo ambalo kwangu naliona ni sahihi,"amesema.

Pia amesema anafahamu kuwa TFS wanasimamia hifadhi nyingi za misitu ya asili. "Binafsi kwa hapa Magamba pamenivutia sana , kuna maporomoko ya maji yanayotiririka kwa mpangilio ambao umapengwa na Mungu ukapangika.

"Kuna eneo ambalo unaweza kukaa na kuiona Wilaya yote ya Lushoto na Korogwe.Video ya Nimenasa itakuwa mtata sana,"amesema Amini huku akisisitiza kutambua fursa ambayo amepewa na TFS kwa ajili ya kwenda kutengeneza video yake hiyo.

Amini amesema kuwa video ya wimbo wa Nimenasa itatoka siku za hivi karibuni."Nawashukuru sana TFS kwa kunipa nafasi hii, nitoe rai kwa wasanii wenzangu kuhakikisha wanarekodi video zao hapa hapa nchini Tanzania."

Pia amesema TFS wamethibitisha namna wanavyotamani kuona wasanii wa fani mbalimbali ikiwemo ya Bongo Fleva wanarekodi video zao katika mazingira ya nyumbani.

"Wanazo hifadhi nyingi za misitu inayovutia na msanii anaweza kuchagua eneo ambalo anataka kwenda kurekodi kulingana na maudhui ya kazi aliyonayo,"amesema Amini.

Hata hivyo pamoja na maelezo hayo ya Amini ukweli ni kwamba msitu wa Magamba umeficha siri kubwa ya Amini na Linna .Siri hiyo itawekwa wazi baada ya kukamilika kwa video hiyo.
 Msanii wa Bongo Fleva Amini Mwinyimkuu akiwa na Linna Sanga wakati wakirekodi video ya wimbo wao mpya wa Nimenasa.Wasanii hao walikwenda hifadhi ya msitu wa asili wa Magamba uliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya kurekodi video hiyo chini ya ufadhili wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu (kushoto) akiwa amemshikia kipaza sauti msanii Linna Sanga wakati wakirekodi video ya Nimenasa katika msitu wa Magamba uliopo Lushoto mkoani Tanga.
Msanii maarufu katika muziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu akizungumzia video yake ya Nimenasa ambayo ameirokodi kwenye msitu wa Magamba .
Wasanii Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga wakiendelea kurekodi wimbo wao mpya wa Nimenasa katika msitu wa Magamba ambao upo chini ya usimamizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini