Katika kuboresha huduma zake kwa wananchi, Mahakama ya Tanzania imeamua kuanzisha Mahakama inayotembea (Mobile Court) ili kuendelea kusogeza huduma za kimahakama karibu zaidi na wananachi. Lengo la kuanzishwa kwa kwa huduma hii muhimu pia ni kuwapunguzia wananchi gharama za kufuata huduma za Mahakama na Kuongeza imani ya wananchi kwa Mahakama.
Mahakama inayotembea ni kitendo cha Mahakama kuhamisha huduma zake na kuzitolea katika sehemu mbalimbali ndani ya mamlaka husika. Dhana hii pia inamaanisha kuwa Mahakama inaweza kuhamisha huduma zake na kuzitolea sehemu mbalimbali kwa kutumia gari maalumu lenye chumba kilichotengenezwa mithili ya ofisi ya Hakimu, kinachoweza kutumika katika kusikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi.
Gari litakalotumika kutoa huduma za Mahakama lina nyenzo zote za kimahakama kama vile sehemu ya kusikilizia mashauri, vitendea kazi vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya kisasa ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kama vile kamera, mfumo wa matangazo (PA system) na mwavuli kwa ajili ya kivuli na viti vya kupumzikia wateja. Aidha, mahakama hii ni gari maalumu lenye sehemu mbili (2) Chumba cha hakimu ambacho kitakuwa na meza ya hakimu, meza ya wadaawa, meza ya karani/mpiga chapa, Televisheni, Kompyuta “Printer”, Kabati la kutunzia majalada, Vyombo vya kurekodi mashauri na vifaa vya kutangazia (vipaza sauti) pamoja na chumba cha faragha.
Historia ya Mahakama inayotembea Tanzania
Dhana hii ya Mahakama inayotembea ilikuwepo tangu miaka ya 1920 ambapo Mahakama Kuu kwa wakati huo ilitumia behewa la treni kutoa huduma za kimahakama kwenye ukanda ambao treni ilipita. Sababu za kuhamisha mahakama zilikuwa kumfuata shahidi kwa sababu ni mgonjwa au kuwapunguzia gharama mashahidi au iwapo kielelezo hakihamishiki kirahisi.
Huduma zitolewazo katika Mahakama inayotembea
Aidha, huduma zitakazotolewa na Mahakama inayotembea ni pamoja na kupokea, kusajili na kusikiliza mashauri, kutoa taarifa za mashauri, kutoa fomu za viapo na kuthibitisha nyaraka mbalimbali. Huduma nyingine zitakazotolewa ni kufanya usuluhishi kwa wadaawa na kutoa elimu kuhusiana na masuala mbalimbali ya Mahakama.
Aina za mashauri yanayosikilizwa katika Mahakama inayotembea
Kama ilivyo kwa Mahakama tulizozizoea, Mahakama inayotembea itasikiliza mashauri ya aina zote yanayosikilizwa na Mahakama za Mwanzo kama vile migogoro ya ndoa, madai, mirathi pamoja na jinai. Mahakama hii itasikiliza mashauri katika operesheni maalumu.
Ratiba ya utoaji huduma
Baada ya kuanzishwa kwa Mahakama inayotembea, Mahakama ya Tanzania inatarajia kutoa huduma kwa kufuata Kalenda na ratiba maalumu pamoja na taratibu zilizowekwa. Ratiba (causelist) zitatoa taarifa na maelekezo ya siku na muda ambao shauri litasikilizwa.
Utekelezaji Hukumu (kukaza hukumu)
Utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama inayotembea utafanywa katika Mahakama za kawaida katika eneo/mamlaka husika. Mfano, hukumu iliyotolewa na mahakama inayotembea katika kituo cha Bunju utekelezaji wake utafanyikia kwenye Mahakama ya Mwanzo Kawe.
Haki ya Kukata Rufaa katika Mahakama inayotembea
Mhusika yeyote katika shauri asiyeridhika na uamuzi wa Mahakama inayotembea ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama ya juu. Kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo, mhusika anaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Wilaya kwa kufuata taratibu zilizopo. Kwa upande wa Mahakama ya Wilaya mhusika anaweza kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Faida zitakazopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mahakama inayotembea
Baadhi ya faida zitakazopatikana kutokana na Mahakama ya Tanzania kuanzisha Mahakama inayotembea ni pamoja na kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au kuondoa kabisa mlundikano wa mashauri mahakamani. Mahakama inayotembea pia itasaidia kuwapunguzia gharama wananchi za kufika Mahakamani kufuatilia haki zao na kupitia Mahakama hii ustawi wa jamii utaimarika. Aidha, Mahakama hii itakuwa ni fursa pekee ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi kwa kuwa wananchi hawatatumia muda mrefu kufuatilia haki zao kwa kuwa Mahakama inayotembea uitarahisisha upatikanaji wa haki.
Maeneo yatakayohudumiwa na Mahakama inayotembea
Kwa kuanzia, huduma hii itatolewa katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza. Katika mkoa wa Dar es salaam, huduma ya Mahakama inayotembea itatolewa katika maeneo ya Bunju “A” (kwenye viwanja vya ofisi ya Serikali za mitaa), Kibamba (kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni), Chanika (pembeni ya kituo kipya cha Polisi Chanika) na Buza (eneo la kituo cha mabasi Buza).
Katika Mkoa wa Mwanza, huduma za Mahakama inayotembea zitatolewa katika maeneo ya Buhongwa (eneo la wazi karibu na kituo cha Polisi Buhongwa), Igoma (eneo la kuegesha Malori Igoma-Terminal Trucks ground) na Buswelu katika Viwanja vya Soko Buswelu.
Licha ya kuanzisha huduma ya Mahakama inayotembea kwa baadhi ya maeneo nchini, Mahakama ya Tanzania inao mpango la kutanua wigo wa utoaji wa huduma kwa njia ya magari maalum katika mikoa mingine hapo baadaye ili kuendelea kusogeza huduma za kimahakama karibu zaidi na wananchi na kurahisisha upatikanaji wa haki.
Rais azindua Mahakama inayotembea
Akizindua Mahakama inayotembea hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kuanzisha huduma hii kwa kuwa itasaidia kutoa haki kwa wananchi wengi na kuitaka Mahakama kuongeza idadi ya magari hayo ili kufikia maeneo mengi zaidi nchini.
Akizungumza wakati wa sherehe za kilele cha wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini, Mhe. Rais pia aliipongeza Benki ya Dunia kwa ufadhili wa ununuzi wa magari hayo ya Mahakama inayotembea.
“Nakupongeza sana Mhe. Jaji Mkuu pamoja na Watumishi wote wa Mahakama kwa ujumla kwa maboresho ya Mahakama yaliyofanyika na vilevile napongeza uanzishwaji wa huduma ya Mahakama inayotembea kwani itawasaidia wananchi kutatua migogoro mbalimbali” alisema Mhe. Dkt. Magufuli.
Hata hivyo, Mhe. Rais aliitaka Mahakama kuelekeza huduma hiyo katika kutatua matatizo ya wananchi hususani wanawake wajane ambao wanahangaika muda mrefu kufuatilia mirathi hatua ambayo wakati mwingine inawasababisha kukosa haki zao za msingi.
“Maombi yangu, huduma hii iwasaidie pia wanawake ambao wengi wanahangaika kwa muda mrefu kushughulikia mirathi, ikibidi liwepo gari maalum ambalo ikiwezekana awekwe Jaji/Hakimu mwanamke kwa ajili ya kuwasaidia wamama wajane kuhusu masuala ya mirathi,” alisisitiza Mhe. Rais.
Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumzia Mahakama inayotembea wakati wa siku ya Sheria nchini alisema Mahakama zinazotembea zitasaidia kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi hasa sehemu zisizo na Mahakama, kusikiliza kesi na kuzimaliza.
“Katika dhana hii mpya ya Mahakama inayotembea mahakama itahamishia shughuli zake katika chumba maalumu kilichotengenezwa ndani ya gari lakini kuna huduma zote muhimu kama ilivyo ofisi au “chambers” ya hakimu ambapo itasikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi”, alisema Jaji Mkuu.
Alisema dhamira ya Mahakama baadaye ni kuwa na magari ya aina hii nchi nzima kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi kwa mfano jamii za wafugaji na wavuvi ili kuwapunguzia wananchi wote kero. Mahakama hizi zitakuwa chini ya mamlaka ya Mahakama husika za Wilaya na Mwanzo na Mahakimu walioteuliwa kuzisimamia wamepatiwa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya kuhudumia wateja (customer care). Aliongeza kuwa Mahakama inayotembea inatarajiwa kuwa kimbilio la wananchi wengi kwa huduma nzuri zitakazotolewa katika mahakama hizo.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN MAGUFULI AKIZINDUA MAHAKAMA INAYOTEMBEA WAKATI WA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI NA SIKU YA SHERIA. WA TATU KUSHOTO NI JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA NA KULIA KWA RAIS NI SWPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MHE. jOB nDUGAI AKIFUATIWA NA ALIYEKUWA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. PROF. PALAMAGAMBA KABUDI. KUTOKA KUSHOTO NI MWAKILISHI WA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA TEMEKE, SOPHIA MJEMA AKIFUATIWA NA MUWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI BIBI BELLA BIRD.
MUONEKANO WA NDANI GARI LITAKALOTOA HUDUMA ZA MAHAKAMA INAYOTEMBEA INAYOTARAJIWA KUANZA KUFANYA KAZI HIVI KARIBUNI.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments