VIDEO CHAFU YA NGONO YAIMUIBUA GWAJIMA...AJIPANGA KUJIBU MAPIGO | ZamotoHabari.


*Atuma salamu kwa TCRA kuchukua hatua kwa aliyesambaza 

*Asema anachafuliwa kwasababu mwakani ni mwaka wa uchaguzi

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amejitokeza hadharani kujibu mapigo baada ya kusambaa video chafu ya ngono inayomuonesha akiwa kitandani akifanya mapenzi na mwanamke.

Video ya Askofu Gwajima ilianza kusambaa jana asubuhi na kadri saa zilivyokuwa zikienda ndivyo habari yake ilivyozidi kusambaa na kuwa gumzo. Katika mitandao ya kijamii kwa sasa habari ya mjini ni Gwajima.

Akizungumza leo Mei 8, 2019 Askofu Gwajima amesema amewaita waandishi wa habari ili kuzungumzia tukio ambalo lilitikisa siku za nyuma na akaamini limekwisha na kwamba alijua vita imeisha na aliamua kuweka silaha chini.

"Ukiona mtu amebeba makombora yake basi unachokifanya na wewe unachukua silaha zako.Nimeona leo nizungumze na watu wangu wa Ufufuo. Kuanzia jana niliona mtandao fulani wa Oroginali Isragramu ambaye alianza kupost picha zinaoonesha mambo yasiyofaa dhidi yangu.Nilianza kuona tangu asubuhi na baada ya hapo niliamua kufuatilia kwa kufanya utafiti kwanza maana nilitakakujua nani yuko nyuma ya hili. Nataka kurudisha adabu maana naona anataka kunizoea tena,"amesema.

Amefafanua kwanza video hiyo haina ukweli wowote bali ni ya kutengeneza na inaonesha lengo ni kumchafua ili kumnyima sauti ya kuzungumzia maovu lakini ukweli yeye atabaki imara kuliko ilivyokuwa sasa.

"Kuna mkakati wa kunichafua, hivi hata tukio hili lingekuwa la kweli iweje mambo ya chumbani yaletwe hadharani? Huwezi kuchukua mambo ya faragha ya watu wazima waliokuwa chumbani na kisha ukaanza kuyasambaza mtandaoni.

"Nia ya mtu huyo sio nzuri na hata sheria ya nchi inaleza wazi kuna picha za aina fulani ambazo hazitakiwi kuonwa hadharani .Tayari ninayo RB kama hatua ya awali ambayo nimechukua, pia naitaka TCRA imkamate mtu huyo na sheria ichukue mkondo wake.Nitashangaa kama TCRA itakaa kimya bila kumchukulia hatu myu ambaye ameamua kumchafua,"amesema Askofu Gwajima.

Amongeza aliyesambaza video hiyo anajua kabisa Askofu Gwajima ana mke, anajua ana watoto wakubwa, anajua siku za karibuni alikuwa Marekani alikokwenda kuhubiri Injili na anajua anayo makanisa 400.

"Hivyo aliyefanya kitendo cha kusambaza video hii ashindwe kwa jina la Yesu. Kwanini mimi ? Najua mwakani ni mwaka wa uchaguzi hivyo aliye nyuma ya hilii anatumia mbinu chafu kunichafua ili kuninyima sauti.Na sasa kinachoonekana yanaletwa matukio ya kunizima lakini sitakubali na nitajibu mapigo,"ameseam Askofu Gwajima.

Hata hivyo amesema katika video hiyo kuna picha za wasichana tofauti tofauti ambazo zimeunganishwa ili kumchafua na baadhi ya picha zinaonesha mwili mwingine na kichwa ni kingine huku akifafanua kwa mwanaume mwenye akili hawezi kujipiga picha mwenyewe na kisha kusambaza.

"Kwa mfano katika hizo picha iko moja ambayo nilipiga nikiwa na familia yangu ambayo sikuwa nimevaa shati na ilikuwa ni mwaka Oktoba 20, 2018 .Kupiga picha na familia yangu sio tatizo lakini kinachoonekana watu wameamua kuunganisha picha ili kuninyamazisha,"amesema Askofu Gwajima.

Hata hivyo amesema waliosambaza video hiyo badala ya kumchafua wamedhirisha yeye ni mwanaume rijali na kwamba kila kila silaha itakayofanyika juu yake haitafanikiwa .

"Kuanzia Jumapili hii nitaanza kujibu mapigo ...nataka iwe kama Jumali zilee ambazo watu walikuwa wanasikiliza Gwajima anatasema kitu gani.Dunia ina watu wa ajabu ambao wanapenda kuwekea wenzao mambo ambayo hayapo.
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima aalipokuwa akizungumza na Vyombo vya Habari leo,kuhusu kujibu mapigo baada ya kusambaa video chafu ya ngono inayodaiwa ikimuonesha akiwa kitandani akifanya mapenzi na mwanamke.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini