MAKAMU WA RAIS AZINDUA RIPOTI YA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM | ZamotoHabari.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira mara baada ya kuizindua katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (kushoto) mara baada ya kuzindua ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
…………………. 




Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua ripoti ya hali ya Hali ya Mazingira nchini Tanzania ambapo ripoti hiyo imetaja sababu mbalimbali ikiwemo ya kasi ya ongezeko la watu na ukuaji wa maendeleo unachangia kwa sehemu kubwa uharibifu wa mazingira.

Akizungumza leo Mei 6,2019 wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mama Samia amesema ripoti hiyo imefanywa kati ya Serikali ya Tazania na Benki ya Dunia na lengo ni kuangalia kwa kina kuhusu hali ya mazingira nchini na hatua za kuchukua katika kutafuta ufumbuzi wake. 

Amefafanua ripoti ioanesha kuwa kasi ya ongezeko la watu na kasi ya ukuaji wa uchumi nchini unachangia uharibifu wa mazingira, hivyo ni jukumu la Watanzania pamoja na watalaam wa kada mbalimbali na wadau wa maendeleo kuangalia namna bora itakayowezesha idadi ya watu inayoongezeka na ukuaji wa uchumi hauwi sehemu ya kuharibi mazingira nchini. 

“Ripoti inaposema ukuaji wa uchumi na kasi ya ongezeko la watu ndio sababu za uharibifu wa mazingira, lazima watanzania na watalaamu kwa ujumla kutusaidia kutafuta ufumbuzi wake.Kama kasi ya ongezeko la watu ni sababu sasa tufanyeje ?Inaana nusu ya watu ipungue, au kasi ya ukuaji wa uchumi ambayo nayo inatajwa kama sehemu ya chanzo cha kuharibu mazingira inachangia. 

“Ni lazima Watanzania tuangalie namna bora itakayofanikisha mazingira yanatunzwa na shughuli za maendeleo na kasi ya ukuaji wa watu inaendelea.Ndani ya ripoti imeonesha namna ambavyo rasilimali za Tanzania namna ambavyo zinaharibiwa. 

“Imeonekana kuwa matumizi mabaya ya maji, uharibifu wa hali ya hewa, kilimo na mambo mengine kadhaa yanachangia kuharibu mazingira.Watalaamu wanayo nafasi ya kushauri na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kulinda mazingira yetu,”amesema Makamu wa Rais. 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba amesema kuwa “Leo ni siku muhimu kwa watu tunaohusika na mazingira kwasababu tumezindua ripoti ya hali ya mazingira ambayo imefanywa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.Ripoti hii inaeleza hali ya uchambuzi nchini Tanzania. 

“Chimbuko la ripoti hii ni mazungumzo ambayo tumekuwa nayo muda mrefu na wenzetu wa Benki ya Dunia pamoja na wadau wa maendeleo kuhusu namna gani nchi yetu inapata maendeleo kwa namna endelevu zaidi. Tunaposema maendeleo endelevu maana yake ni mchakato mzima wa kutafuta maendeleo ambayo yatadumu. Tutafute maendeleo huku tukitunza mazingira. 

“Ripoti inaonesha hali halisi ya uharibifu wa mazingira na bahati nzuri inaelekeza namna bora na nzuri ya kuhakikisha tunalinda mazingira yetu.Tumeona kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira na wakati huo huo tunayo matumaini makubwa kwani kuna hatua ambazo zimependekezwa ndani ya ripoti hiyo ili kuhakikisha tunabaki salama katika eneo la mazingira. 

Amefafanua katika ripoti hiyo kuna sababu nyingi ambazo zimetajwa kama sehemu ya kuchangia uharibifu wa mazingira na sababu kubwa inatajwa kasi ya ongezeko la ukuaji wa watu na kasi ya ukuaji wa uchumi.Pia amesema kilimo cha umwagiliaji maji nacho kimetajwa moja ya sababu ya kuharibifu wa mazingira. 

Kuhusu mapendekezo ambayo yametajwa ndani ya ripoti hiyo , Waziri Makamba kuna mapendekezo manne ambayo yametolewa na pendekezo namba moja ni kuhakikisha taasisi za uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa hali ya hewa zinaimarishwa kuongeza udhibiti. 

Makamba amefafanua katika ripoti inaonesha watu 26000 wanafariki dunia ka mwaka kutokana na uharibifu wa hali ya hewa huku akieleza kuwa kila dakika misitu inayoharibiwa ni urefu wa kiwanja cha mpira, hivyo kuna kila sababu ya kuendeleakuchukua hatua ili mazingira yabaki salama. 

Hata hivyo amesema baada ya kuzinduliwa kwa ripoti hiyo, kinachofuata ni mjadala katika kuichambua na kisha kuwekwa mikakati mbalimbali ambayo itaifanya nchi yetu iendelee kutunza mazingira yake hasa kwa kuzingatia kuna hatua nyingi zinachukuliwa kuhakikisha mazingira yabanaki salama.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini