RAIS WA SHIRIKISHO BARAZA LA TAIFA FALME ZA KIARABU (UAE) AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA AFRIKA | ZamotoHabari.



Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akifungua Mkutano wa Bunge la Afrika leo nchini Afrika Kusini

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi amefungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika ulioanza leo Mei 6,2019 jijini Johannesburg,Afrika Kusini kwa kukutanisha wabunge kutoka nchi 54 barani Afrika.

Akitoa hotuba yake, Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi alisema Bunge la Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) zimekubaliana kushirikiana na Bunge la Afrika katika kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi barani Afrika.

“Uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bara la Afrika umekuwa mkubwa,tumekuwa tukisaidia mambo kadha wa kadha barani Afrika,tunataka kuona usalama unazidi kuimarika Afrika,kwani bila usalama katika nchi zetu hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa”,alisema Dr. Amal.

“Masuala ya vitendo vya kigaidi yana athari kubwa,tunatakiwa kwa pamoja kushirikiana kuyatafutia ufumbuzi ili wananchi wetu wawe salama lakini pia kuwa na suluhisho la kudumu juu ya wakimbizi wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani,tunafurahi kuona wakimbizi wakirudi kwenye nchi zao kwa amani”,alisema.

Kwa upande wake,Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang alisema ili ushirikiano na umoja madhubuti unahitajika ili kufikia suluhu za kudumu juu ya masuala ya amani na usalama barani Afrika.Ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika litakalofungwa Mei 17,2019 umekwenda sanjari na wabunge 26 wapya wa bunge la Afrika kutoka nchi mbalimbali kuapishwa.

Kauli mbiu ya Bunge la Afrika mwaka huu ni "2019 mwaka wa Wakimbizi,wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani : Kuelekea kupata masuluhisho ya kudumu katika kulazimishwa kuhama makazi katika Afrika".Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa Bunge la Afrika likifunguliwa leo..Tazama hapa chini

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akitoa hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019 Midrand, jijini Johannesburg,Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa hotuba yake Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019.

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (katikati),Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang na washiriki wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa Umoja wa Afrika.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wakiimba wimbo wa Umoja wa Afrika.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (kulia) na viongozi mbalimbali wa bunge la Afrika wakiwa katika ukumbi wa bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa ukumbini.
Bunge linaendelea.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Aliyekuwa Mjumbe wa Uongozi wa Bunge la Afrika Dr. Bernadette Lahai kutoka Sierra Leone akitoa tamko na ujumbe wa mshikamano barani Afrika.


Wabunge wakiwa ukumbini.

Wabunge wapya wa bunge la Afrika kutoka Swaziland wakila kiapo bungeni leo. Hao ni miongoni mwa wabunge 26 kutoka nchi mbalimbali walioapishwa leo.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika wakiendelea kiapo Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.

Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini