Mbwana Samatta afunguka kuhusu tuzo aliyoshinda | ZamotoHabari.

Nahodha wa Taifa Stars anayekipiga katika klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta amefunguka mara baada ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2019 anayecheza soka nchini Ubelgiji (Ebony Shoe Award). 


Utakumbika usiku wa May 6 kuingia May 7 2019 Samatta alifanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2019 anayecheza soka nchini Ubelgiji. 


"Nina furaha kuwa mshindi wa tuzo hii lakini siwezi kuwa mchoyo wa fadhila kwani nafahamu kuwa nisingeweza kufikia hatua hii Leo bila kuwa na msaada wa wachezaji wenzangu,benchi la ufundi,mashabiki na kila mmoja ndani na nje ya club ya KRC Genk," ameeleza. 


Ameendelea kwa kusema "Pia kwa wote ambao walinipigia kura ya mimi kuwa mshindi,nawashukuru kwa mchango wao mkubwa kwangu katika msimu huu. Pia nipende kuwashukuru watanzania wenzangu ambao siku zote wako pamoja nami katika maombi na sapoti yao kwa namna moja ama nyingine,". 



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini