Na Woinde Shizza, Michuzi TV
Wananchi Wa Wilaya ya Arumeru wapo mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) baada ya kujengewa mochwari Mpya ya kisasa na serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mkuu wawilaya hiyo mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Cosmas Kalasala alisemakuwa chumba hicho chakuhofadhia maiti mpaka kiishe kitagarimu kiasi cha shilingi milioni 160.
Alisema kuwa mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 80% na kwamba wanatarajia kukamilisha ujenzi huo hivi karibuni ili wananchi waweze kutumia jengo hilo waondokane na usumbufu wa kwenda kuhifadhi miili ya marehemu nje ya Wilaya.
Mkuu wawilaya hiyo Jerry Muro alisema serikali ya awamu ya tano imeona tatizo hili la ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti hivyo wakaamua watoe fedha za mfuko wa jimbo na kijengea chumba hicho katika hospital ya wilaya ya Arumeru
"Unajua fedha hizi za maendeleo ya mfuko wa jimbo ni za maendeleo ya wananchi wa Meru hivyo tumefata utaratibu wa kushirikisha wananchi tukachukua fedha hizi kwa ajili ya kuwajengea wananchi wa Meru chumba cha kuhifadhia miili ya marehemu ndugu zao"alisema Muro.
Alisema kuwa wananchi hao walikuwa wanapata taabu sana pindi ndugu zao wanapofariki kwani hospital ya wilaya ilikuwa haina huduma hiyo hivyo walikuwa wanalazimika kwenda kuhifadhi miili ya marehemu ndugu zao katika hospital ya mkoa ya Arusha (Mount meru hospital ) ambapo ni zaidi ya kilometa 20 kutoka hospital hiyo ya Wilaya.
DC Muro alisema jengo hilo linalojengwa ni kubwa na litakuwa na uwezo kuhifadhi miili 45 hadi 50 ya marehemu kwa wakati mmoja na kwamba wanatarajia kulizindua rasmi na Mwenge wa Uhuru mapema Mwezi Juni mwaka huu.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kalasala akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru jinsi chumba hicho cha kuhifadhia maiti kilivyofikia
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kalasala akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru jinsi chumba hicho cha kuhifadhia maiti kilivyofikia
Mkurugenzi wa Jalmashauri ya Meru akifafanua jambo katika ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ya kukagua ujenzi wa mochwari hiyo ulipofikia
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema jengo hilo la kuhifadhia maiti litasadia sana wananchi wa wilaya yake kwani walikuwa wanapata taabu sana ya kusafirisha miili pindi ndugu zao wanapofariki dunia.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments