Mwili wa Dkt. Mengi wapokelewa na Maelfu Dar | ZamotoHabari.

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi,  umewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kupokelewa na maelfu ya waombolezaji.

Mwili huo unapelekwa kwa msafara hadi Hospitali ya Jeshi Lugalo, iliyopo Mwenge kwa ajili ya kuhifadhiwa ambapo kesho utaagwa katika Ukumbi wa Karimjee, Posta,  na kupelekwa kwao Machame kwa mazishi yatakayofanyika Alhamisi.


Maelfu ya waombolezaji wenye nyuso za huzuni, wengi wao wamemwaga machozi wakati mwili wa mfanyabiashara huyo aliyeaga dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 Dubai katika Falme za Kiarabu, ukiwasili.


Watu waliojipanga barabarani kuupokea pia wamejikuta wakiangua vilio kutokana na kuguswa na msiba huo mzito kwa Tanzania na Afrika
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini