Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
RAIA wa Uingereza, anayeishi Mikocheni jijini Dar es Salaam, Derick Tweedley (85), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha sh. Milioni 717 mali ya Gulam Dewji.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, amedai mbele ya Hakimu Mkazi. Maira Kasonde leo Jumanne, Mei 7, 2019 kuwa, Desemba 9 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alijipatia USD 300,000, ambazo ni sawa na Sh milioni 717milioni kutoka kwa Gulam Dewji.
Imedaiwa kuwa mshitakiwa huyo alijipatia kiasi hicho cha fedha baada ya kumdanganya Dewji kuwa atahamisha umiliki wa kiwanja namba 16066 na 7902 kwenda kwenye Kampuni ya Mohamed Enterprises (Tanzania) wakati akijua kuwa sio kweli.
Mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo
Yalimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho watakao wasilisha fedha taslimu sh. Milioni 353.5 kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi hadi Mei 20, mwaka huu, itakapotajwa.

Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments