Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS Dk. John Magufuli amewasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga na kutoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Dk.Reginald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 akiwa Dubai.
Dk. Magufuli amefika katika viwanja hivyo saa 4:30 asubuhi ambapo baada ya kufika waombolezaji wengine waliokuwa msibani hapo walisimama ambapo alikwenda moja kwa moja hadi lilipo jeneza lenye mwili wa Dk.Mengi. Baada ya hapo Rais alikwenda kukaa na kisha kuanza kusikiliza viongozi wa dini ambao walikuwa wakiendelea kutoa mahubiri kuhusu kifo cha Mengi na mchango wake kwa Watanzania.
Mbali ya Rais Magufuli , pia viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria kuaga mwili wa Dk.Mengi. Pia marais wastaafu nao wamehudhuria pamoja na kada nyingine za makundi mbalimbali ya Watanzania,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, pamoja na Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma wakiwa katika ukumbi wa Karimjee, kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi.
Hata hivyo wakati Rais anafika viwanja vya Karimjee, Askofu wa CCT Nelson Kisare alikuwa akiendelea kutoa mahubiri kabla ya kufanya maombi kwa ajili ya mzee Mengi.Wakati anahubiri Askofu Kisare amesema kuwa Dk.Mengi amekuwa mmoja wa Watanzania wachache ambao wametumia fursa zilizopo khakikisha anatatatua changamoto.
Amesema Dk. Mengi enzi za uhai wake amefanya mambo mengi makubwa na ya mfano wa kuigwa na kutaka jamii ya Watanzania kuiga matendo mema ya mpendwa wetu."Dk.Mengi kupitia biashara zake amekuwa akilipa kodi na kodi hiyo imeleta maendeleo kwa Watanzania, mzunguko wa fedha zake umekwenda kwa watanzania,na wapo ambao wamepata ajira kupitia biashara zake.Hivyo ametoa mchango mkubwa na amegusa maisha ya wananchi mbalimbali.
Askofu Kisare amesisitiza yale ambayo yana sifa njema na matendo mema ambayo amefanya Dk.Mengi maisha yake ya hapa duniani ni vema kila mmoja wetu akatafakari.
Wakati huo huo Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Father Kitima kabla ya kutoa maombi kwenye shughuli za kuaga mwili wa Dk.Mengi, amesema kuwa Dk.Mengi alikuwa karibu sana na Kanisa Katoliki kwa kushiriki katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo zinahosu Kanisa hilo ."Kanisa Katoliki Tanzania limeguswa na msiba wa Dk.Mengi.Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Arusha aliyefanya kazi kwa karibu na Mzee Mengi amesema rafiki yake amemuacha lakini ameacha alama kutokana na mchango wake.
Mjane wa Marehemu Dkt. Mengi, Jacqueline Mengi akiwa pamoja na watoto wa Marehemu.
"Imani ya Dk.Mengi , sisi tunaamini maisha ya mwanadamu , ni maisha yaliyoungwanishwa na maisha ya muumba wake. Katika Injili ya Yohana sura ya 11 tunaelezwa jinsi Yesu anavyoeleza kifo hakina ushindi kwa mwanadamu. Tunapofurahia kazi nzuri za Dk. Mengi katika kuwafanya watanzania wakutane kupitia vyombo vya habari na kuhimiza kufanya mambo mema , ni jukumu letu kuenzi na kuendeleza mema ambayo ameyatenda,"amesema.
Pia Futher Kitima amesema binadamu hapa duniani anakabiliana na nguvu za uovu na anapambana nazo na hivyo wanahitaji msaada wa Mungu. Dk.Mengi ametenda mengi lakini bado tunayo kila sababu ya kuzidi kumuombea na kubwa zaidi kuungana na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments