ROSE NDAUKA AWASHAURI WASANII WA BONGOMOVIE KUBORESHA SOKO LA FILAMU. | ZamotoHabari.


         Na.Khadija seif,Globu ya jamii.

MSANII wa tasnia ya filamu nchini Rose Ndauka amefungua biashara ya saloon jijini Dar es salaam.

Ndauka amesema ukimya wake katika filamu kwa muda mrefu umetokana na majukumu ya kifamilia pamoja na biashara ambayo ameianzisha hivi karibuni ya saloon ya kike na kiume.

"Rose ni yule yule na kadri navozidi kukua  majukumu ndio yanazidi ila bado niko vizuri na ninapenda kazi yangu ya sanaa kwani ndio ilionitambulisha kwenye ramani ya Tanzania na watu wanaifahamu kupitia sanaa", alisema ndauka.

Hata hivyo ameeleza ukimya huo pia umemuwezesha kujinoa upya na kurudi kwenye tasnia akiwa mpya kwani ameweza kuyafanyia kazi malalamiko ambayo mashabiki kila kukicha hutoa na kusema kwa sasa filamu nyingi hazina ubora na zinapelekwa sokoni pasi na ubunifu na utofauti kwenye kazi hizo.

Pia amewapa ushauri wasanii na watengenezaji wa filamu kuboresha kazi zao ili ziweze kupewa thamani katika jamii na kupata wanunuzi wengi kwani soko bado lipo na wasanii wazuri bado wapo .

Aidha ndauka amewapa rai mashabiki wake kuwa waendelee kununua kazi zake na kumshauri pale anapokosea kwani bila wao hata Leo hii asingeweza kufungua biashara zingine kutokana na kuwa wadau wakubwa wa kazi za filamu na kununua pia .



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini