UBALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania umesema umesikitishwa na kifo cha mfanyabishara maarufu na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dk.Reginald Mengi huku ukielezea namna ambavyo walikuwa wakishirikiana naye katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza leo Mei 7,2019 wakati wa kuaga mwili wa Dk.Mengi katika viwanja vya Kamrijee jijini Dar es Salaam, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frediric Clavier amesema kifo cha Dk.Mengi ni pigo kwa Taifa la Tanzania na kwamba ubalozi wa Ufaransa umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hiyo.
"Ubalozi wa Ufaransa pamoja na wafanyakazi wake wote, tumesikitishwa na kifo cha Dk.Mengi.Binafsi kwangi mimi naweza kusema nilipata bahati kwani nimeshauriana naye mambo mengi yenye kulenye kulenga kuimarisha taasisi mbalimbali.Tulibadilisha mawazo kuhusu shughuli za kibiashara,"amesema Balozi Clavier.
Amefafanua kuna mambo mengi ambayo yamefanywa na Dk.Mengi wakati wa uhai wake na kwamba amekuwa akikumbuka vikao vyao mbalimbali ambavyo amekaa na Dk.Mengi kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na kubwa zaidi anakumbuka tabasamu lake lililojaa upendo wakati wote.
"Dk.Mengi alikuwa akishirikiana na Ubalozi wa Ufaransa lakini pia tunatambua pigo kubwa ambalo Taifa la Tanzania limepata kutokana na kuondokewa na mtu muhimu.Ubalozi wa Ufaransa tutakumbuka namna ambavyo Mengi alijitoa kwa ajili ya kusaidia makundi ya watu wasiojiweza,"amesema.
Amesisitiza "Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kumuomba Mungu ampumzishe ndugu yetu mahala pema peponi.Amina."
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments