Serikali Yawalipa Wananchi Fidia Bonde la Mto Ruhila | ZamotoHabari.


Wizara ya Maji imelipa jumla ya Shilingi 1,913,832,491 ikiwa ni fidia kwa wananchi waliokuwa na makazi kando kando ya Bonde la Mto Ruhila ambalo ni chanzo cha maji cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo, Wananchi hao wamekuwa wakifuatilia malipo yao kwa miaka 15 iliyopita tangu mwaka 2003. Malipo hayo yamefanyika kwa awamu tatu (3); awamu ya kwanza kiasi kilicholipwa ni Shilingi 500,000,000/= na awamu ya pili na ya tatu kiasi kilicholipwa ni Shilingi 1,413,832,491.

Kazi hiyo ya kuwalipa wananchi hundi zao imesimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA).

Idadi ya wananchi waliolipwa fidia ni 723. Hata hivyo, idadi ya wananchi wapatao 80 hawakujitokeza kuchukua hundi zao ambazo bado zipo katika Ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA),wananchi waliobaki wanaombwa kufika katika ofisi hizo kuchukua hundi zao.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini