WAFANYAKAZI WAWILI WA CAMEL WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA | ZamotoHabari.

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 

MFANYAKAZI wa Kampuni ya mafuta ya Camel David Leole na mwenzake Khalid Said, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashitaka matatu likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh. milioni 181.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Groly Mwenda amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde kuwa kati ya Januari 2016 hadi Machi 2018 katika sehemu tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa la wizi wakiwa watumishi wa kampuni hiyo.

Imedaiwa kuwa siku na mahali hapo, washitakiwa hao waliiba Sh.181,181,350 iliyoingia mikononi mwao kutokana na nafasi zao za kuajiliwa.

Aidha ,washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha fedha kwa kuziingiza katika akaunti ya Leole ya benki ya NMB huku wakijua fedha hizo zimetokana na zao la kosa la wizi.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 28 mwaka huu itakapotajwa tena. Washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kuwa kosa la utakatishaji fedha halina dhamana.




Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini