Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bashiru Ally amehoji juu ya watu wanaodai kuwa uchumi wa Tanzania haukui na kueleza kuwa isingeweza kununua ndege nyingi kwa wakati mmoja.
Dkt Bashiru Ally ametoa kauli hiyo hivi karibuni katika ziara yake ya kikazi Mkoani Pwani katika Wilaya ya Kibaha huku ikiwa ni muendelezo wa vikao vya Bunge jijini Dodoma, na kueleza kuwa wako baadhi ya Wabunge, wanaodai uchumi wa Tanzania unashuka.
"Nchi ambayo uchumi wake umekufa inawezaje kununua ndege, tena kwa fedha taslimu?, nchi ambayo uchumi wake haukui inajenga vituo vya afya kila kata nchi hii?.
"Tunasambaza umeme hadi vijijini kwenye nyumba za tembe, watoto wanasoma bure, huchumi haukui?", amesema Dkt Bashiru.
Kwa sasa Wabunge jijini Dodoma wanaendelea na majadiliano ya Makadirio ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo zaidi ya Trilioni 33.1 zimetengwa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments