Boda Boda Ambaka Abiria Wake Aliyekuwa Akienda Kwa Mpenzi Wake | ZamotoHabari.

2Mhuhudumu mmoja eneo la Rachuonyo kaunti ya Homa Bay alikimbilia usalama wake baada ya kikundi cha vijana kutaka kumuuwa kwa kumpiga mawe

Imeripotiwa kuwa mshukiwa alimbaka mteja wake wa kike aliyetaka ampeleke kwa mpenziwe usiku wa Jumanne Juni 12.


Wahudumu wenzake wa bodaboda wanasemekana kughadhabishwa na kitendo hicho cha Vincent Okoth ambapo pia walitaka kumuadhibu kwa kuwachafulia sifa.

Mhudumu wa bodaboda ambaka mteja aliyetaka ampeleke kwa mpenziwe
Mhudumu wa bodaboda ambaka mteja aliyetaka ampeleke kwa mpenziwe
Chifu wa kijiji hicho Joshua Owiti alisema Okoth alimbaka mwanamke huyo aliyekuwa amesafiri kutoka Narok kwenye chumba kimoja ambacho kimesalia mahame katika kijiji cha Jwelu.

Mwathiriwa alipelekwa katika hospitali ya Homa Bay ambapo ilithibitika kuwa alibakwa baada ya kufanyiwa vipomo.

Kulingana na taarifa za edaily, mshukiwa alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Othoro huku uchunguzi zaidi ukianzishwa dhidi yake.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini