Na Charles James,Globu ya jamii
Katika kukuza vipaji vya vijana katika Mkoani Dodoma, Diwani wa Kata ya Buigiri iliyopo Wilaya ya Chamwino Kenneth Yindi ameandaa mashindano ya mpira wa miguu yatakayoshirikisha tmu mane za kata hiyo.
Mashindano hayo yaliyopewa jina la Buchimwe Cup 2019, yatazinduliwa kesho na Mkurugenzi wa Michezo Nchini, Ado Komba ambapo mshindi wa kwanza atajnyakulia Kombe, Seti Moja ya Jezi na kiasi cha Sh 100,000 taslimu.
" Lengo la mashindano haya ni kukuza vipaji vya vijana wetu, Michezo imekua Ajira kubwa Duniani kote hivi sasa, hivyo kama Diwani nimeoana nianzishe mashindano haya ambayo naamini yatatumika kama fursa kwa wachezaji wetu kuweza kupata Timu kubwa zaidi ya hizi walizonazo sasa.
"Tunashukuru Wizara ya Michezo chini ya Waziri Mhe Harrison Mwakyembe kwa kutuunga mkono katika kufanikisha mashindano haya bila kuwasahau Chama Cha Soka Mkoa (DOREFA)," amesema Yindi.
Ameongeza licha ya Ligi hiyo kuchezwa pia ameandaa mafunzo ya uamuzi kwa waamuzi waliyopo ndani ya Kata yake yenye viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Soka nchini TFF.
" Kwa kushirikiana na wenzetu wa Dorefa tumeandaa pia mafunzo haya kwa waamuzi na watakaofuzu watakabidhiaa vyeti vya kuhitimu, lengo letu ni kukuza Michezo kwenye Mkoa wetu, " amesema Yindi.
Amesema kitendo cha Rais Magufuli kuwaletea ujenzi wa uwanja wa Kisasa wa Michezo uliopo eneo la Nzuguni ni heshima kwao hivyo hawana budi kuhakikisha sasa wanaandaa vijana wazawa kukua kimichezo ili kuweza kunufaika na uwanja huo.
" Rais Magufuli tunampongeza sana kwa kutupa heshima kubwa ya uwanja wa kisasa, sasa ni jukumu letu sisi wasaidizi wake kuwaandaa vijana wetu kimichezo ili wanufaike na zawadi hii ambayo Rais ametupa sisi watu wa Dodoma,"
Yindi amesema pia kutakua na zawadi Kwa mshindi wa pili na wa tatu, mfungaji na mchezaji bora wa mashindano, kipa bora pamoja na mchezaji bora wa kila mechi.
Diwani Yindi akizungumza kuhusu namna alivyojipanga kukuza vipaji kwenye kata yake
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments