Na Ripota wetu ,wa Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu amezindua boti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko.
Pia Kanyasu ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi misitu nchini.
Akizungumza leo Jumamosi Juni 29,2019 wakati wa uzinduzi boti hizo Kanyasu ameitaka TFS iongeze bidii kwa kubuni matumizi sahihi ya boti hizo."Kumekuwa na matumizi tofauti na yaliokusudiwa hivyo inabidi kubuni matumizi na kuwa na nidhamu katika matumizi yaliyokusudiwa" amesema Kanyasu.
Amesema boti hizo zitasaidia kuthibiti uvunaji holela wa mikoko ambayo ni muhimu kutokana na uhifadhi wa bahari.
Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TFS Meneja Kanda ya Mashariki, Caroline Malundo amesema boti hizo zitatumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko na kuongeza kumekuwa na changamoto nyingi ndani ya hifadhi ikiwemo ukataji wa mikoko na kufanya kilimo cha mpunga.
"Tumekuwa na changamoto nyingi ndani ikiwemo ukataji wa mikoko,kilimo cha mpunga ndani ya delta ya Rufiji pamoja na bandari 77 zisizo rasmi" amesema Malundo.
Kwa upande wa Mmiliki wa kampuni ya Sam and Anzai Boat Builders iliyotengeneza boti hizo Samweli Luenje amesema wametengeneza boti tatu kwa gharama ya shilingi 600 milioni ambapo tayari moja imeshaanza kazi kati eneo la Nyamisati.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) baada ya kuzindua boti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduaboti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko ambapo ametumia nafasi kuipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi misitu.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments