Dj Khaled hajafurahia kuona Album yake imeshindwa kufika namba 1 na kudondokea namba 2 kwenye chart za “Billboard Hot 100” inaripotiwa kuwa ameikasirikia Label yake.
.
Vyanzo vya karibu vimeuambia mtandao wa Pagesix kuwa Dj Khaled alienda kwenye ofisi za Epic Records kuangalia data za mauzo ya Album yake na alipokuta zinaonesha kuwa Album ya #FatherOfAsahd imekuwa ya pili alipandisha hasira na kuanza kuilalamikia label.
.
“Dj Khaled huwa anaonekana mtu wa furaha muda wote lakini ana hasira sana” Chanzo Kimoja kimefunguka. “Hakutaka kabisa kukubali kuwa namba 2”
.
Mbali ya Promotion kubwa ikiwemo kutokea kwenye Kipindi cha SNL (Saturday Night Live) na Collaboration Kubwa, Album ya Khaled imeshika namba 2 nyuma ya Igor, Album mpya ya Taylor The Creator (Ambaye pia ni msanii wa Sony, label Mama ya Epic Records inayomsimamia Khaled)
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA




0 Comments