Skyner: Sina Muda na Wanae | ZamotoHabari.

MREMBO mwenye figa matata aliyepata umaarufu kupitia Bongo Movies, Skyner Ally ‘Skaina’ ameweka wazi kuwa, hana muda wa kupoteza kuwafikiria wanaume kwani akili yake inawaza biashara tu.

Akizungumza na Amani, Skyner alisemaa alichojipangia kwa sasa maishani mwake, badala ya kupiga soga, umbeya, majungu na wanaume, anajishughulisha katika biashara zake ikiwemo ya nguo.

“Mimi mwili wangu siwezi kuutumia kwa wanaume, niko zangu bize na biashara hata huo muda wa kufanya mambo ya kipuuzi sina,” alisema Skyner ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego.’
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini