Genge la Wabakaji INDIA Lawanyoa Vipara Mama na Mwana Waliokataaa Kubakwa | ZamotoHabari.

Watu wawili wamekamatwa katika jimbo la Bihar nchini India baada ya kundi la wanaume kuwanyoa vipara wanawake waili kama "adhabu" ya kugomea kubakwa.

Kundi hilo la wabakaji, ambalo lilimjumuisha kiongozi mmoja wa kijiji, liliwavamia mama na mtoto wake ndani ya nyumba yao wakiwa na nia ya kuwabaka, polisi wamethibitisha.

Baada ya wanawake hao kugoma kubakwa, waliwashambulia na kuwanyoa nyweke zote kichwani na kuwatembeza kijiji kizima.


Polisi wanasema wanawasaka wanaume wengine watano waliohusika kwenye tukio hilo.

"Tulichapwa hovyo na fimbo. Nina majeraha mwili mzima. Na binti yangu pia ana maheraha," mama aliyeshambuliwa amelieleza shirika la habari la Ani.

Wanawake hao wamesema nywele zao zilikatwa mbele ya kijiji kisima.


Kujaribu kubaka ni kosa la kijinsia nchini India, lakini shambulizi lilofuata la kuwanyoa nywele kuwachapa na kuwatembeza kijiji kizima linaonesha nguvu ya wanaume kwenye jamii.

Kinachotia hofu zaidi ni kuwa, kundi la wabakaj hao lilikuwa likiongozwa na na afisa wa serikali - mwakilishi aliyeschaguliwa ili kulinda maslahi ya watu wake na si kuwashambulia.

Uthubutu wa watuhumiwa hao unaonesha ni kwa namna gani katika baadhi ya maeneo nchini India wat hawana woga wa sheria.

Awali ya yote, masikini na wale ambao mbao wapo kwenye makundi yaliyotengwa ni ngumu kwao hata kuwashawishi polisi kufungua mashtaka yao.

Malalamiko yao hupelezwa pasi na umakini na endapo yakipelekwa mahakamani hukutana na msururu wa kesi zinazoendeshwa taratibu, na mwishowe watu wenye ushawishi wanaweza kuachiliwa hata kwenye kesi za mauaji.

Hasira ya jamii na ghadhabu ambazo huinekana baada ya tukio kuripotiwa huisha baada ya muda mfupi tu,

Kinachohitajika ni hatua kali tena za uhakika kutoka kwa mamlaka ili kupatiwa haki kwa waathirika na kurudisha utawala wa sheria katika maeneo ya mbali na vijijini nchini humo
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini