Raia tisa wa Tanzania pamoja na raia wawili wa Msumbiji wameuawa na watu wasiojulikana huku Watanzania wengine sita wakijeruhiwa vibaya katika kijiji cha Mtole kilichopo upande wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni, IGP Saimoni Siro amefika mkoani Mtwara kufuatilia tukio hilo lililotokea Juni 26, 2019 na kusema msako unaanza mara moja kwa kushirikiana na Serikali ya Msumbiji ili kuwakamata watu waliohusika na mauaji hayo.
Wakizungumzia tukio hilo majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Ligula wamesema kuwa watu hao waliofanya mauaji walikuwa saba na waliwalaghai wananchi kwa kuitisha mkutano na kuanza kuwashambulia.
Wajeruhi hao wameiomba Serikali kuhakikisha inawakamata wauaji hao. Mauaji hayo yalitokea wakati Watanzania hao kutoka Kijiji cha Kihamba upande wa Mtwara wakiwa kijijini hapo kwa shughuli za kilimo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments