Na Charles James wa Michuzi Tv- Dodoma
TAASISI ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa imefungua na kuzindua Baraza jipya la wafanyakazi ikiwa ni mara ya kwanza yangu kuanzishwa kwa Hospitali hiyo kubwa nchini.
Akizungumza na wafanyakazi wa Hospital hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula ametoa rai kwa Wafanyakazi wa baraza hilo kuwajibika na kufanya kazi kwa kujituma zaidi pamoja na kuonesha uzalendo kwa Wagonjwa.
“Tunajifunza kila siku,kwa hiyo nyie mlioteuliwa mtuwezeshe,haki haipo bila wajibu,na kila mmoja akijituma atatizimiza wajibu wake,mimi sikumbuki kutumwa na napata shida kum-push mtu,na lazima tutengeneze Mechanism ya watu kufanyakazi bila kutumwa. Hakuna kazi ya neema na ibada tunayo fanya kama hii, Mtu ana Stress zake,ana shida,hana hela lakini unamfariji,unamtibu,mwisho wa kazi saa 9 ukifanya kazi mpaka saa 11 au saa 1 jioni una dhambi gani.” Amesema Dk Chaula.
Aidha amewataka wafanyakazi kuwa Wepesi katika kutekeleza Majukumu yao na kutowakwaza wagonjwa na wananchi kwa ujumla hivyo ni jambo la busara kupeana Moyo katika kazi ngumu na yenye wito ya utabibu na kumtegemea Mungu katika changamoto wanazokumbana nazo .
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Dokta Chaula amesema upendo na huruma ni jambo la Muhimu kwa Maisha ya Binadamu kwani ni Moja ya Kujenga Marafiki wengi na kusema kuwa hakuna mtu mdogo katika maisha kila mtu ana mchango wake na kinachotofautisha ni Madaraka na Mamlaka tu ila binadamu wote ni sawa..
“Kwa makusudi tu mtu anakuja halafu anatoka analia ofisini kwako unajisikiaje,lazima tupendane tuhurumiane tukitengeneza system ya namna hii katika maisha yetu tutakuwa na marafiki wengi kuliko maadui,tusameheane”Alisema.
Kwa upande wake Katibu wa Baraza la wafanyakazi mkoa wa Dodoma,ambaye pia Mjumbe Taifa wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali kanisa la Waadventista Wasabato ,[ATAPE] Bw.Mchenya John amesema amesema wataendelea kuyafanyia kazi maelekezo yote muhimu yaliyotolewa huku akizungumzia namna walivyofanya mchakato wa uanzishaji wa Chuo wa Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa akitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa awamu ya nne Dokta.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha uanzishaji wa Hospitali hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dokta Alphonce Chandika amesema taasisi hiyo ina takriban miaka mitatu tangu ianzishwe na walikuwa hawajaunda Baraza la Wafanyakazi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafanyakazi lakini kwa sasa idadi imejitosheleza na wameona kuwa na umuhimu wa kuwa na Baraza ambapo tayari na katiba na mkataba wa Baraza hilo ilishatengenezwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Zainab Chaula akizungumza na watumishi wa Hospital ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Watumishi wa Hospital ya Rufaa ya Benjamini Mkapa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Zainab Chaula wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye Taasisi hiyo
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments