Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua pampu mpya ya maji iliyofungwa katika kijiji cha Mpapula Halmashauri ya Wilaya Mtwara mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya maji.
Waziri Mbarawa akielekea eneo ilikofungwa pampu mpya ya maji katika kijiji cha Mpapula mkoani Mtwara ambapo huduma ya maji imerejea baada ya pampu hiyo kuungua kwa muda na alipofika Waziri wa Maji mwaka jana aliagiza pampu mpya inunuliwe haraka ili wananchi wapate majisafi na salama.
……………………..
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) ameridhishwa na kurejea kwa huduma ya maji katika kijiji cha Mpapula kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara baada ya wananchi hao kufungiwa pampu mpya na kuanza kufanya kazi.
Waziri aliyasema hayo leo mara baada ya kufika katika kijiji cha Mpapula na kukuta pampu ya maji mpya iliyofungwa inafanya kazi baada ya pampu ya zamani kuungua mwaka jana.
Pampu hiyo iiliharibika mwaka jana na haikuwa katika sehemu ya Mkataba wa Mkandarasi hivyo kupelekea wananchi kukaa kwa muda mrefu bila ya kupata majisafi na salama hadi Waziri wa Maji alipokuja kujionea tatizo hilo na kuahidi kuwanunulia pampu.
“Serikali iliahidi na imetekeleza” alisema Waziri Mbarawa wakati akikagua pampu hiyo. Mradi huo wa Mpapula unahudumia kata 2 ya Mpapula na muungano na wananchi wapatao 5953 wananufaika na mradi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda alisema kununuliwa kwa pampu hiyo kutasaidia kuondoa kilio cha shida ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Mpapula, na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutochimba katika njia ambazo mabomba yanapita. Kufanya hivyo kutasaidia kutunza mabomba hayo yasipasuke na kufanya huduma ya maji kuwa endelevu kwa wananchi.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments