Na Woinde Shizza Michuzi Tv , Arusha
BARAZA la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kaskazini limefanya ukaguzi na kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo mkoani Arusha ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki.
Ukaguzi na utolewaji wa elimu,unakuja kutokana na changamoto ya wajasiriamali wadogo wa Mkoa wa Arusha kugeuza vifungashio vya plastic kuwa vibebeo vya kubebea bidhaa sokoni.
Hivyo leo Juni 22,2019 Baraza hilo limefanya ukaguzi katika Soko la Kilombero pamoja Mbauda ambapo limetumia nafasi hiyo kuwapa elimu wafanyabiashara wa masoko hayo pamoja na kupiga marufuku utumiaji wa vifungashio hivyo Kama vibebeo
Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini Lewis Nzari amesema wamefanya ukaguzi wakagundua kuwa wafanyabiashara hawa wadogo baada ya kunyimwa kutumia mifuko ya plastic (Maliboro) wameamua kutumia vifungashio vya plastic kubebea vitu kitu ambacho ni kinyume cha Sheria.
"Kweli kunavituko tumepita uku masokoni na kufanya ukaguzi tukakuta wafanyabiashara wamegeuza vifungashio kuwa vibebeo sasa kitu tulichofanya tumeamua kuwapa elimu na wameelewa na tumetoa onyo kuwa kuanzia Kesho tukija tusikute wanaendelea kutumia vifungashio hivyo kama vibebeo na tukikuta mtu anafanya hivyo tutamchukulia hatua kali za kisheria "Novatus Mushi mkaguzi wa mazingira .
Amebainisha kwakuwa wamegundua tatizo hilo wataendelea kupita katika masoko mengine yote yaliopo mkoani hapa kwa ajili ya kukagua pamoja na kutoa elimu kuhusiana na suala hilo.Ameongeza kuwa wananchi wataelimishwa kuhusu aina za mifuko mbadala yenye ubora unaotakiwa kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa miongozo.
Amefafanua katika kwenda sambamba na sera ya viwanda wananchi watapata wasaa wa kufahamu tathmini ya athari kwa mazingira ili kuhakikisha sera Tanzania ya viwanda inafanikiwa .
Aidha wakitoa maoni wafanya biashara hao wameiomba Serikali kuwatafutia vifungashio mbadala vya kuweka vimiminika kama, barafu na nyama ilikupunguza usumbufu wanaoupata.
Mkaguzi wa mazingira Novatus Mushi akionyesha wananchi vifungashio ambavyo havitakiwi kufanywa vibebeo
mfanyabiashara wa soko la kilombero akiuliza swali
Meneja wa NEMC kanda ya kaskazini Lewis Nzari akiendelea kuwapa elimu wafanyabiashara wa soko la kilombero .
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments