Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
WAKAZI wapatao 2073 katika Jiji la Arusha wamesajiri laini zao katika kipindi cha siku saba cha maadhimisho ya utumishi wa Umma ambapo TCRA ilitumia nafasi hiyo kutoa elimu na kuhamasisha watumiaji wa mawasiliano kusajiriwa laini zao kwa njia ya vidole.
Aidha wananchi wapatao 4, 757 wameweza kuchukua fomu na kujisajiri kwa ajili ya vitambulisho vya Uraia ,vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho, NIDA na kuweza kusajiriwa laini za simu ,ambapo miongoni mwao walisajiri laini mpya 417.
.
Akizungumza katika Viwanja vya Kilombero ,jijini hapa,Kaimu Mkuu wa Kanda wa TCRA Landa ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salumu amewataka watumiaji wa mawasiliano ya simu kuendelea kusajiri laini zao ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza mara baada ya mchakato kufungwa Desemba 30,mwaka huu.
Imelda ameonya matumizi ya laini za simu zisizosajiriwa kuwa ifikapo Desemba 30 mwaka huu laini hizo zitazimwa na hatua kali zitachukuliwa kwa atakayetumia lini bila kusajiriwa.
Amesema katika zoezi hilo la kutoa elimu kwa mtumiaji wa mawasiliano waliambatana na maofisa wa NIDA Idara ya Uhamiaji, huku makampuni ya simu kutoka Vodacom,Tigo,Halotel,TTCL na Airtel zikishiriki katika kuhakikisha wananchi wanasajiri laini huzo kwa njia ya Vidole.
"Kwa ujumla mchakato umefanyika kwa mafanikio kwani wananchi 4757 walichukua fomu za kusajiri vitambulisho vya uraia, huku laini zipatazo 2073 zilisahiriwa kwa njia ya vidole , laini mpya zilizonunuliwa na kusajiriwa zilikuwa 417,"amesema Imelda
Awali Mkuu wa Kitengo cha Huduma za watumiaji bidhaa za mawasiliano,Zakayo Ringo amesema zoezi hilo limekuwa na mwitikio mkubwa na kuwataka waliokosa fursa ya kusajiri vitambulisho vya NIDA na Kilombero wataendelea kusajiriwa katika ofisi za NIDA zilizopo Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wakati usajili huo kuendelea katika viwanja vya Kilombero na Chuo cha Uhasibu Arusha wamelalamikia utaratibu mbovu wa NIDA katika kuhakiki namba za vitambulisho na kusababisha wananchi kutumia muda mrefu kukaa kwenye foleni jambo ambalo linazorotesha zoezi hilo la kusajili.
Kaimu Mkuu wa Kanda wa TCRA Landa ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salumu
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments