WAKULIMA LEMKUNA WAIOMBA SEREKALI KUWAONGEZEA ENEO LA KILIMO CHA UMWAGILIAJI | ZamotoHabari.


Shamba la zao la mpunga katika skimu ya umwagiliaji ya Lemkuna Iliyopo wilayani Manyara mkoani simanjiro, ambapo Mpunga huo upo tayari kwa ajili ya mavuno. 
Banio linaloruhusu maji kwenda katika mashamba yaliyopo katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Lemkuna Wilayani Simanjiro, ambapo imelezwa na wakulima ambao niyo watumiaji kuwa maji hayo yametoka katika mto ruvu na bwawa la maji la mto wa mungu. 
…………………. 

NA MWANDISHI MAALUM –SIMANJIRO 
Wakulima katika skimu ya Umwagiliaji ya Lemkuna iliyopo katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba serikali kuwaongeazea eneo linalotumika katika kilimo cha umwagiliaji kwa sasa lenye ukubwa wa Hekta mia tatu (300) mbali na zaidi ya hekta elfu kumi (10,000) zilizoendelezwa kwa kilimo cha Hicho. 

Akiongea na waandishi wa Habari kwa niaba ya wakulima katika katika skimu hiyo, Mwenyekiti wa chama cha wakuliwa Lemkuna Uwale Bw. Stanley Msuya amesema kuwa kutokana na kilimo hicho kuwa na mafaniko na faida kubwa katika jamii inayozunguka maeneo jirani, kumekuwa na mwamko mkubwa wa vijana wa kizazi kipya katika maeneo hayo kuwa na hari ya kujiajiri kupitia sekta ya kilimo, lakini maeneo mengi yamekuwa yakimilikiwa na watangulizi au wazazi wao jambo ambalo limepelekea vijana hao kukosa maeneo ya kufanya shunguli za kilimo. 

“kilimo hiki cha umwagiliaji kimekuwa na faida kubwa kwetu sisi wakulima hasa baada ya serikali kupitia tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutujengea miundo mbinu ya umwagialia, kipato cha mkulima mmoja kabla ya maboresho na kupatiwa mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, mkulima aliweza kupata gunia za Mpunga kwa mfano kuanzia kumi na tano (15) mpaka ishirini (20) kwa heka moja, lakini kwa sasa mkulima anaweza kupata hata gunia thelathini na tano (35) mpaka hamsini (50) unaweza kuona namna ambavyo kilimo hiki kina faida, Hivyo tunaiomba serikali kufanya upanuzi wa eneo hili kwani vijana wanahitaji sana kufanya shughuli za kilimo.” Alisisitiza Bwana Msuya. 

Akiongelea baadhi ya Changamoto wanazokabiliana nazo wakulima katika Skimu hiyo, Bw. Msuya alisema kuwa Chama hicho kimekuwa hakina kifaa za kuvunia zao la mpunga na ili kukabiliana na changamoto hiyo kipo kwenye mchakato wa kupata mkopo kupitia Bank ya kilimo na Bank ya NMB nchini ili kuweza kununua mashine hiyo na kuweza kuinua wakulima wadogowadogo kwa kuchangia katika upatikanaji wa pembejeo za kilimo na kuongeza mtaji. 

Skimu ya kilimo cha umwagiliaji Lemkuna ipo katika kanda ya umwagiliaji ya Dodoma, inayohusisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini