Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepatwa na mshangao baada ya kuwakuta mahabusu 11 wa mauaji ambao walifutiwa kesi na mahakama, kuwepo Kituo cha Polisi Gogoni, kwa muda wa miezi sita.
Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho kilichopo Wilaya ya Kipolisi Kimara, Wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo kwa lengo la kuangalia utendaji wa Polisi kituoni hapo, mara baada ya kuwahoji mahabusu 32 kituoni hapo akakutana na mahabusu hao ambao baadhi yao walifungwa miaka saba Gerezani.
“Kituo hiki cha Gogoni kwa mujibu wa taarifa nilizo nazo kinaongoza nchini kwa kukaa na mahabusu kwa muda mrefu, sasa hili la mahabusu 11 waliofutiwa kesi kuwepo kituoni hapa hii si sawa, na pia linanishangaza,” alisema Lugola.
Amesema viongozi wa Polisi Wilaya wamempa taarifa ya uwepo wa mahabusu hao, amewapa maelekezo kulifanyia kazi tukio hilo, naye ameahidi kuichukua changamoto hiyo na uongozi wa Wizara kuifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
“Kuna malalamiko ya vituo kukaa na watuhumiwa bila kupelekwa mahakama na kituo hiki kinaongoza kwa kukaa na mahabusu kwa muda mrefu na leo Juni 23, 2019 nimekuta mahabusu 32, wakiwemo mahabusu hawa 11 ambao wameniletea mshangao,” alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, lengo la ziara zake ni kukagua na kuona ufanisi wa namna Jeshi la polisi linavyotoa huduma kwa wananchi na kuwasikiliza maoni ya wananchi juu ya huduma wanazozipokea kutoka kwa jeshi hilo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments