Afande Sele "Wanangu, Nikifa Mnichome Moto" | ZamotoHabari.



Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele amewataka watoto wake kwamba akifariki wahakikishe anachomwa moto.
Afande Sele amewataka watoto wake wasimamie hilo kwa kuwa hiyo ni zawadi ambayo anaona itamfaa kutokana na malezi kwa watoto wake hao.

Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii ameadika

“Kila wakati nikipata nafasi ya kuongea na hawa binti zangu wawili huwa nawakumbusha kwamba yote ninayowatendea chini ya jua ni wajibu wangu na ni haki yao lakini kitu pekee kikubwa kwangu wanachoweza kunilipa ni wao kuhakikisha kuwa siku yangu ya mwisho ikifika wasiruhusu kivyovyote mwili wangu kuzikwa/kufukiwa udongoni bali zawadi iliyobora kwangu watakayopaswa kunipa ni kuhakikisha mwili wangu unateketezwa kwa Moto na kubakia majivu ambayo ndio watayazika ardhini na kubakia kama alama ya pale nilipo lala mimi ule usingizi mzito na usiokua na ndoto…’maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua’….usifosi tufanane.,” na wasipo fanya hivyo atapita Morogoro yote nyumba hadi nyumba akiwalaani wakazi wote wa huko.
_
Afande Sele awali aliwahi kutoa taarifa ya kutaka asizikwe na achomwe moto huku akidai hana dini hivyo hataki ahusishwe na dini yoyote.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini