Na Mwandishi wetu, Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi bwana Juma Homera ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa kwanza; unaotekelezwa na kampuni ya ukandarasi kutoka china ya CRCEBG; kutokana na mradi huo kuonekana kusua sua ambapo umeunganisha umeme katika vijiji vinne tu kati ya vijiji ishirini na tisa vilivyopaswa kuunganishiwa huduma hiyo katika kipindi cha miezi mitatuiliyopita ya utekelezaji wa mradi
Bwana Homera ameonyesha hali hiyo wakati wa kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini katika vijiji vya Mnyaki, Kapalala B na Society katika halmashauri ya nsimbo wilayani mpanda
Akizungumza na watumishi wa TANESCO walioambatana na Meneja msaidizi wa REA awamu ya tatu mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amewataka kuongeza kasi ya uwashaji umeme vijiji kwani wananchi wanasubiria huduma hiyo
“Ukitazama mikoa mingine wako mbali sana ila hapa mmlelala, sasa hivi tunaandaa ilani ya chama cha mapinduzi tutaawaambia nini wananchi” alisema Homera .Aliongeza kuwa atawasilina na Waziri mwenye dhamana ili kuona kama kuna uwezekano wa kuweka usimamizi wa ziada katika utekelezaji wa mradi huo
Akitoa sababu za kucheleweshwa kwa uwashaji wa umeme katika vijiji hivyo Meneja Msaidizi kutoka kampuni ya ukandarasi ya CRCEBG Mhandisi Arnold Nzali amesema wamepata changamoto ya uhaba wa vifaa ambapo wamelazimika kuagiza kutoka nchini China
Nzali amesema mradi unahitaji vifaa vingi kwa wakati mmoja hali iliyoshindikana kupatikana kwa pamoja hapa nchini na hivyo kumlazimu Meneja wa mradi huo kuelekea nchini China kuvifuata .Hata hivyo amesema baadhi ya nguzo za umeme zimeanza kuwasili hivyo kazi inaendelea
Naye Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Katavi Mhandisi Dotto Chacha amesema kwa kila wiki mkandarasi anapaswa kuwasha umeme katika vijiji vitatu .Amesema kwa sasa mkandarasi amekwisha washa vijiji 4 kati ya 29 sawa na asilimia 18
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments