Kila mwanadamu huwa mipango yake ambayo umejipangia mwenyewe katika maisha yake, na ikumbukwe pia kama ambavyo tujuavyo ya kwamba mafanikio ni matokeo yatokanayo na mipango na mikakati thabitia mbayo mtu ameipanga jinsi ya kutekeleza mipango hiyo.
Ukweli ambao upo bayana ni kwamba mipango mingi hufa katika hatua za awali kabisa yaani mtu anapowaza tu anajikuta umeingiwa na roho ya kushindwa, roho ya kutokujiamini kuwa kupitia wazo lake anaweza kufanya kitu au anaweza kubadilisha kitu katika maisha yake, watu wengi wamefungwa na roho za uoga na roho za kutokujiamini.
Pia tafiti nyingi zinasema kwa siku mwanadamu huwaza mawazo mengi sana yale ambayo ni hasi na chanya pia, lakini changomoto kubwa huja katika namna ambavyo mtu atanavyoamua kuchukua hatua stahiki juu ya mawazo chanya anayowaza kila wakati.
Wengi tunawaza vizuri sana lakini mawazo hayo hufa pasipo kwenda katika hatua ya utekelezaji, wengi wetu tumejikuta tukighairisha kufanya mambo ya msingi kwa sababu tumekuwa ni wavivu wa kuchambua mawazo yetu ya msingi kwa kina zaidi, wengi tumekuwa ni mabigwa wa kujipa majibu hasi kabla jambo hilo halijaenda katika kulitekelezaji.
Unakuta mtu ana wazo fulani la msingi lakini changamoto inakuja katika kugeuza mawazo hayo kuwa kitu halisi, hapo ndipo palipo na ukakasi pamoja na kipangimizi kisichokuwa na tija.
Hivyo kama una kiu ya kupiga hatua za mafaniko, unatakiwa kukumbuka mipango mingi ya kimafanikio hufa mapema sana kama mtu huyo hatakuwa makini katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.
kila wakati ikumbukwe ili kuweza kufanikiwa kimaisha unatakiwa kukumbuka ya kwamba kila kitu tunachokiwaza tunatakiwa kuchukua hatua stahiki juu ya kitu hicho na si kuishia kuwaza tu.
Mwisho naomba nimalize kwa kusema mafanikio ya haki yako ya msingi endelea kusimamia katika mawazo yako.
Na: Benson Chonya.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments