CHUO CHA MWALIMU NYERERE CHAVUMBUA MFUMO WA UMWAGILIAJI WA KISASA | ZamotoHabari.

CHUO Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeeleza kujipanga vyema katika kutoa elimu kwa njia ya kisasa katika mifumo mbalimbali ya sayansi na teknolijia,ikiwemo mfumo wa simu ya kiganjani kurahisisha mawasiliano na elimu kuwafikia walengwa kwa wakati . 

Akizungumza na Michuzi tv wakati wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa (maarufu maonesho ya sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Bakari Ramadhani ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho amesema kukua kwa sayansi na teknolojia kumepelekea maboresho ya vitendea kazi pamoja na miundombinu katika sekta ya kilimo. 

"Mfumo wa umwagiliaji ni rahisi na uhakika haraka kutokana na simu kutumika Kama nyenzo ya umwagiliaji ambapo mkulima anaweza kupakua programu itakayomuwezesha kufanya umwagiliaji hata akiwa mbali na shamba lake," 

Aidha, mbunifu huyo ameeleza mfumo huo umetengenezwa takribani wiki moja kupitia mafunzo waliopata chuo cha Mwalimu Nyerere katika somo la tehama na mawasiliano. "Changamoto nilizopata ni kutopata vifaa vya kutengeneza mfumo huo kwa haraka hapa nchini," 

Pia ametoa wito kwa wanafunzi kusoma masomo ambayo yatakua na manufaa kwa nchi yao ili kuendelea kufikia uchumi wa viwanda .



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini