WAZIRI HASUNGA AJA NA MKAKATI WA KUKUZA KILIMO NCHINI | ZamotoHabari.

Na Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati   ifikapo mwaka 2025 imeelezwa kuwa ni lazima iwekeze kikamilifu katika kilimo hifadhi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika kilimo.

Hayo yamebainisha Jijini Dodoma na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga, wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Kilimo Hifadhi Tanzania.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ikiwamo kufuta kodi nyingi pamoja na kuhamasishaa matumizi ya Teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki katika kilimo.

Amebainisha kuwa ni muhimu kujadiliana pamoja kuhusu sheria kwani hatuwezi kufika uchumi wa kati mwaka 2025 bila kufikia kilimo imara na chenye tija.

“Lazima kuimarishwe mafunzo kwani kilimo nchini bado kipo chini, pia tuongeze utafiti kwakuwa bila utafiti hakuna kilimo na lazima ijulikane kilimo gani kitumike,pembejeo gani zitumike,pia tuongeze uzalishaji wenye  tija,” amesema Waziri Hasunga.

Katika kuimarisha na kuwapa uwezo wakulima amesema Serikali inakuja na mkakati wa bima kwa wakulima lengo likiwa ni kumsaidia mkulima pindi ambapo mazao yake yatakuwa yameharibika shambani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa amesema kama Serikali itawekeza katika kilimo hifadhi basi sekta ya kilimo itafika mbali.

Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM) ameiomba Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo hasa katika utafiti na kufanya mageuzi makubwa katika kilimo hasa katika sheria.

“Sera na sheria zina matatizo makubwa unakuta mkulima natayarisha shamba naanza kulima napalilia halafu wakati wa kuvuna Serikali inaanza kunipangia nikauze wapi sio sawa kabisa hapa ni lazima tutengeneze sheria nzuri” amesema Mgimwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo, Hifadhi Barani Afrika(ACT) Saidi Mkomwa amesema kilimo hifadhi ni kilimo kinachozingatia uhifadhi wa rasilimali udongo na mazingira kwa ujumla.
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza katika warsha ya wadau wa kilimo hifadhi Tanzania iliyofanyika jijini Dodoma leo.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini