DIT YASEMA MAGARI 217 NCHINI YAFUNGWA MFUMO WA KUTUMIA GESI ASILIA, YATAJA FAIDA ZAKE | ZamotoHabari.

Na Said Mwishehe, wa Michuzi TV

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam DIT imesema imeshafunga mfumo wa Gesi asilia katika magari 217 yakiwamo UBER huku akielezea faida lukuki zinazopatikana kwa kutumia gesi hiyo.

Pia DIT imesema iko haja kwa vijana wakitanzania kwenda kujifunza kuhusu namna yakufunga mfumo wa gesi asili nakufanya sevisi kwenye magari hayo kwa lengo la kuhakikisha Tecknolojia hiyo inasambaa katika maeneo mbalimbali nchini na hasa inayopayopatikana gesi kwa wingi.

Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam leo Mhandisi Bosinge ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa taasisi hiyo ametumia nafasi hiyo kueleza baadhi ya faida kwa magari yaliyofungwa gesi asilia.

Mhandisi Bosinge ambaye ndio msimamizi wa karakana ya kufunga mfumo wa gesi asilia kwenye magari katika taasisi hiyo amesema wameaza kufunga mfumo huo mwaka 2008 na hadi sasa wameshafunga magari 2017 na siku chache zijazo wanatarajia kufunga magari 250 kwani muamko umekuwa mkubwa.

Akizungumzia faida zinazopatikana kupitia mfumo huo Mhandisi Bosinge amewaambia wananchi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi katika Banda la DIT kuangalia mfumo huo ambao umekuwa kivutio amesema faida ya kwanza ni gesi asilia ni mali ya watanzania hivyo badala ya kuagiza kutoka nje inapatikana hapa nchini.

Pia amesema matumizi ya endeshaji wa gari mfano yenye cc 2000 unaweza kutumia kilo moja ni Sh.1500 na tunaweza kwenda kilometa 20 mpaka 25 lakini kwa lita moja ya petrol ambayo gharama yake ni 2300 na kwa gari yenye cc 2000 inaweza kwenda kilometa nane na mpaka tisa na hivyo unaweza kuona tofauti ya gharama.

"Ndugu wanahabari kwa mfano gari yenye cc chini ya 1500 ,mtungi wake wa gesi unaulizwaa Sh.19500 ambayo utachukua kilio 13 na unaweza kutembea kilometa 270 ni tofauti na hiyo 19500 ukijaza petrol unatembea sio zaidi ya kilometa 90." Amesema mhandisi Bosinge

Ameongeza kuwa kwa mazingira hayo tunaona namna ambavyo unapunguza gharama kubwa ,na kufafanua kuwa hivi sasa wanauona huduma za usafiri jijini Dar es Salaam kama UBER wengi walikuwa wanatumia hadi Sh.60,000 kea siku kufanya mzunguko wao lakini baada ya kuwafungia gesi asili wanatumia wanatambua zaidi ya kilometa 270 kwa gharama ya msingi mdogo wenye thamani ya sh. 13500 tena kwa siku nzima badala ya 60,000.

Kuangalia hapo tunaona kuna akiba ya Sh.40000 ambayo hiyo inamuwezesha kuitumia katika mahitaji mengine na hivyo kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Bosinge amesema faida ya tatu ni kwenye jijini kwani unapotumia petrol kuna kitu kinaitwa Salfa na Lead na hivyo kusabisha injini kuchoka kwani mafuta yanakuwa yanaganda sana ,hivyo kusabisha injini kuchoka na kufanya sevisi kila baada ya kilometa 3000 lakini ukitumia gesi unaweza kufanya sevisi baada ya kutembea kwa zaidi ya kilometa 9000.

Pia amesema Kwa mazingira inasaidia sana kwani gesi asilia ni rafiki wa mazingira tofauti na kutumia katika magari na kufafanua dunia inapambana kuondoa ozoni leya.

Akizungumzia kuhusu muamko amesema mhandisi Bosinge amesema kimsingi kama Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam wameanza kufunga magari tangu mwaka 2008 na mwanzoni wakipata changamoto kwenye muamko lakini siku za karibuni muamko umekuwa ukingezeka na wananchi wameanza kuelekea.mwanzoni walikuwa wanaogopa kea kudhani gesi italipuka ndani ya magari lakini waliamua kutoa elimu kueleza tofauti wa gesi asili inayotumika kwenye magari na ile ya majumbani LPD.

Amefafanua kuwa gesi hiyo ambayo inatumika kwenye magari ni NCAG ambayo inachimbwa na haina tabia ya kulipuka na kwamba anaendelea kutoa elimu kueleza kuhusu gesi hiyo na ndio maana hivi sasa wameshafunga magari 217 na wanaamini hadi wiki ijayo wanaweza kufunga magari 250.

Kuhusu mwito wake kwa wanaotumia vyombo vya usafiri wa moto yakiwemo magari, mhandisi Bosinge amesema pamoja na faida zote anaamini kwa wananchi hasa wanaoishi Dar es Salaam kupitia maonesho yanayoendelea viwanja vya 77 jijini Dar es Salaam waone umuhimu na faida ya kutumia gesi asilia kwa kuyapeleka magari yao DIT ili kufunguliwa gesi.

Kuhusu gharama za kufunga gesi asilia kwenye magari Mhandisi Bosinge amesema kwa kuanzia CC 0 hadi CC 2000 ni Sh.milioni 1.8 na magari kuanzia CC 2700 mpaka cc 4000 ni Sh.milioni 2.5 na sio zaidi ya hapo na kwamba nimejipanga kupeleka teknolojia hiyo kwa vijana ili waweze kusambaa nchi nzima hasa mikoa yenye ili kuweza kufunga teknolojia hiyo.

"Tumejipanga kufundisha kozi mfupi fupi ambazo DIT inatoa kwa ajili ya kuwaelimisha vijana ikiwa pamoja na kuyafanyia sevisi magari yanayotumia gesi asilia na kufunga mfumo huo." Amesema Mhandisi Bosinge

Amewakaribisha vijana na watu walio tayari sasa kutoka kupata elimu ya kufunga huo mfumo na kisha wakafungue karakana zao.
 Msimamizi wa Karakana ya kufunga magari mfumo gesi asilia katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) Mhandisi Geturu Bosinge akielezea mfumo wa gesi asilia unavyofanya kazi .Gari hiyo iliyofungwa gesi asilia ipo kwenye banda la DIT katika Maonesho ya Biashara Sabasaba yanayoendea jijini.
 Baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la DIT wakipata maelezo kuhusu faida zinazopatikana kwenye magari ambayo wamefungwa mfumo wa kutumia gesi asilia
 Mmoja ya watalaam wa DIT akionesha mtungi wa gesi asilia ambao umefungwa kwenye gari  ndogo iliyopo Banda la DIT katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Gari inayotumika gesi asilia ikiwa imeegeshwa kwenye banda la DIT lililopo katika viwanja vya Sabasaba ambako yanafanyika maonesho ya biashara ambayo yameanza Juni 28,2019
 Baadhi ya wananchi wakiangalia maelezo ya gharama ambazo zinatumika kwa waliofunga mfumo wa gesi asili na zile ambazo zinatumika mafuta ya petrol
Mhandisi Geturu Bosinge wa DIT  akifafanua namna ambavyo mfumo wa gesi asilia unavyofanya kazi


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini