MKUU WA WILAYA ARUMERU JERRY MURO ANUNUA MBUZI WA KISASA KUFANIKISHA HARAMBEE YA KUNUA VIFAA VYA MUZIKI | ZamotoHabari.

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

MKUU  wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amekabidhi mbuzi watatu wa kisasa ambao amewanunua katika mnada wa harambe ya kuchangia ununuaji wa vyombo vya muziki kwa kwaya ya vijana ya Kanisa la AMEC Usharika wa Manyata Halmashauri ya Meru

Muro amenunua mbuzi hao alipokuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo mbali na kuchangia Sh.milioni moja katika harambee   hiyo pia amewanunulia  kina mama wawili wajane mbuzi wa kisasa

 Pia amempatia mtoto mmoja yatima mbuzi kama sehemu ya mbegu aliyopanda katika kuwafariji na hali ya ujane na uyatimawaliokuwa nao

 Aidha Muro amewataka wananchi kutenga muda wa kuwafariji na kuwasaidia watu wasiojiweza katika maisha  kwani kwa kufanya hivyo Mungu atawafungulia milango ya baraka.

"Unajua hata katika vitabu vya dini vinaelezea kusaidia yatima na vinausia kusaidia yatima na ukifanya hivyo utabarikiwa na pia utaongezewa hivyo napenda kuwasihi wananchi kuweni na tabia ya kusaidia, "amesema Muro

Akipokea msaada huo mmoja ya wajane hao alimshukuru  mkuu huyo wa wilaya kwa msaada huo na kueleza kuwa utawasaidia kuendesha maisha kwani watawazalisha na kuuza maziwa.
Picha ya pamoja
Mkuu wa wilaya ya Arumeru akimkabidhi mtoto yatima mbuzi 
Mkuu wa wilaya Jerry Muro akimkabidhi mama mjane Neema Kaaya mbuzi ambae atamsaidia kujikimu .


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini