Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahimu Juma amesema kauli zinazotolewa zinazosema kamata weka ndani zinachangia ongeleko la wafungwa.
Jaji Juma alisema hayo wakati akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kuwaapisha mawakili 720 katika shule ya sheria jijini Dar es Salaam.
“Utasikia kamata weka ndani hayo yote yanachangia ongeleko la magereza tuache sheria ifanye kazi yake,” alisema
Alisema jambo hilo linatakiwa kuangaliwa ni kwamba siku hizi kuna mtindo wa kijamii mfano masuala ya mikataba, mkandarasi kushindwa kukamilisha kazi yake “Utasikia kamata weka ndani hizi zote zinachangia tuache masuala ya kijinai yaende kijinai na masuala yanayohusu mambo ya mikataba yaende kimkataba,”alisema
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments