KILA MTANZANIA ANA WAJIBU WA KULINDA NCHI-DKT BASHIRU | ZamotoHabari.


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Watanzania watakiwa kutambua kuwa kazi ya kulinda uhuru wan chi yetu ni wa kila mwananchi na sio jukumu la Serikali peke yake.

Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali Kakurwa wakati akifungua na kuweka jiwe la msingi katika sherehe za uzinduzi wa boma la “Eunoto”Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja kilichopo ndani ya kata ya Sepeko wilayani Monduli Mkoani hapa ambapo alianza kwa kuwapongeza vijana wa kimasai ambao wameingia katika hatua ya makuzi na kupewa heshima ya kupewa rika na kuitwa Nyangulo.

Alisema kuwa uhuru ambao tulio nao umetokana na mapambano ya wenyeji dhidi ya wageni ambao walitutawala kwa mda mrefu na tukapata ushindi mkubwa na ndio maana nchi yetu ina uhuru na amani na ndio maana tunaheshimika duniani kote.

“ndungu zangu nchi yetu ilitawaliwa na wageni na tabia ya mtawala wa kigeni hutumia mkakati wa kuwagawa anao watawala ili asiweze kumpinga na kumuondoa katika nafasi aliopo ,mkakati mkubwa wa mtawala wa kigeni ni kuwagawa watu wenyeji hivyo tuwe makini na tusikubali kutawaliwa tena na wageni na uhuru wetu na pia tuendelee tulinde amani yetukuendelea kueneza nizamu na ”Alisema Dkt. Bashiru .

Alisema uhuru huu na amani ndio uliosababisha Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta na Rais wetu John Magufuli kuweza kukutana kwa pamoja jiji Mwanza na kuwaarifu dunia kuwa waafrika wote ni ndugu na Afrika ni moja hivyo alitumia jukwaa hilo kuwa wapongeza viongozi hao kwa hutuba walizozitoa kuwa ni nzuri kwani zimelenga kuhamazisha wananchi wao kujenga ujirani mwema ,kudumisha undugu wetu wa umoja Afrika Mashariki pia kukemea migawanyiko inatokana na wanasiasa wasiokuwa na adabu.

“mnajua mji wa Arusha , Kilimanjaro na Tanga mmepakana sana na Kenya ni majirani na mnategemeana katika shughuli mbalimbali za kibiashara ,kijamii na hata za kiutamaduni na mikoa hii pamoja na nchi jirani ya Kenya haina mipaka kwani inategemeana katika shughuli hizi mbalimbali hivyo tuendelee kudumisha umoja huu wan chi zetu pamoja na jumuiya yetu na lengo la sisi wa Afrika ni kufanya nchi zetu za Afrika kuwa moja hivyo naomba niwaambie nyie vijana wa rika la Eunoto (Nyangulo ) muendelee kudumisha umoja huu na muuende na ujumbe kuwa kazi ya kudumisha umoja wetu haija kamilika na itakamilika pale Afrika itakapokuwa moja na mahali pa kuanzia ni kudumisha umoja wa Afrika mashariki”alisema DKT Bashiru.

Akiongelea sherehe hizo kiongozi wa rika ya Eunoto( Nyangulo) Baraka Joseph alisema kuwa sherehe hizi zilizofanyika leo ni za kimila na zinalengo la kuwasimika rika vijana pia sherehe hizi ni kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la kuwapeleka jandoni ( kutairi ) vijana wa rika la Nyangulo,alifafanua kuwa kwa mila ya kimasai zoezi hili linaendeshwa kwa kwa kipindi na huchukuwa kipindi cha miaka saba tangu kufungwa kwa zoezi hilo hadi kipindi cha kufunguliwa

“sisi wamasai tunakuwaga na kipindi cha kufungua zoezi hili tunalolifunga leo tulifungua Rasmi 2012 na tumeliendesha kwa muda wa miaka saba na sasa hivi ndio tumezinduliwa leo sherehe hizi za kufunga kwa iyo tulivyozinduliw a leo tutafanya sherehe hizi kwa muda wa miezi mitatu na ndio tuatafunga rasmi zoezi la kutairi mpaka tena miaka saba iishe ndio tuje tufungue tena upya msimu mungine”alisema Baraka

Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare alipongeza vijana hao kwa hatua waliofikia na kubainisha kuwa waendelee kudumisha yale yote ambayo wamefundishwa na wakubwa wao,alitumia mda huo kutaja changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya hiyo ikiwemo ya ukosefu wa chakula hivyo aliomba serikali iwasaidie kupunguza bei ya mazao ya chakula ikiwemo maindi ambayo alisema kuwa yamepanda kwa kasi kubwa mno.

“kipindi hichi tunaukame mvua hazijanyesha huku kwetu hivyo kunaonekana kunaweza kuwa na tatizola njaa hivyo tunaomba serikali ione namna gani inaweza kutusaidi ,sio wananchi wote ni wafugaji kunawakulima kwa hiyo watateseka hivyo tunaombasana serikali itusaidie na pia mkuu wa mkoa nakupa hili uondoke nalo uone utatusaidiaje na sisi kama kamati ya siasa tutajitaidi kuangalia namna ya kuwasaida”Sanare.

Napenda kumalizia kwa kuwasihi wananchi wa jamii ya wafugaji kupeleka watoto shule kwani ,ili uweze kuongoza vyema lazima uwe na elimu ya kutosha ambayo itakuwezesha kuongoza vyema ,alimpongeza Rais magufuli kwa kutoa elimu bure kwani pia imewasaida watoto wengi wa jamii ya kifugaji ambao walikuwa hawana uwezo wa kulipa ada kuweza kwenda shule.
 Katibu  Mkuu wa chama  chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali Kakurwa akiwa katika picha ya pamoja 
  Katibu  Mkuu akiangalia vijana wa rika la Nyangulo wakiendelea kucheza ngoma zao za kitamaduni ya asili ya kimasai 
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare akizungumza na Wananchi waliofika kwenye sherehe hizo
 Katibu  MKuu wa chama  cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali Kakurwa akiwahutubia wananchi waliohudhuria   katika sherehe za uzinduzi wa boma la “Eunoto”Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja kilichopo ndani ya kata ya Sepeko wilayani Monduli  
Picha ya Pamoja


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini