MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake (pichani juu), wamefurika kwenye banda la TFS kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Undelezaji biashara nchini (Tan Trade) kwenye viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wengi wa wananchi hao ni pamoja na wadau wa misitu na nyuki, wafanyakazi wa umma na binafsi ambao walifika kupata huduma mbalimbali lakini kubwa iliyovutia wengi ni ‘Demo’ ya Mwonekano wa Kijiji cha Mfano kilichohifadhi Mazingira kando kando ya Safu za Milima ya Maporomoko ya Maji kilichopo katika Banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Mwonekano huo wa mfano umevuta hisia za watu wengi kama inavyoonekana pichani na kuinua kiu ya kutaka kujua zaidi kuhusu uhifadhi wa misitu. Sambamba na hilo TFS imetoa ofa ya safari ya kitalii katika Hifadhi ya Msitu Asilia Magamba. safari hii itafanyika tarehe 12 hadi 14 /06/2019 na zitaanzia katika viwanja vya maonesho ya kibiashara (sabasaba) jijini Dar es Salaam na kumalizikia hapo hapo.
Gharama kwa wakubwa ni tsh 171,000 na kwa watoto ni tsh 148,000 tu ikijumlisha gharama ya usafiri, malazi, chakula, tozo ya kuingia hifadhini na gharama ya waongoza wageni.
Malipo yote yatafanyika katika banda la TFS lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya sabasaba.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments