WACHEZAJI wote wa Harambee Stars ya Kenya wamepewa bonasi ya Sh6Mil kwa kuifunga Taifa Stars mabao 3-2 Alhamisi. Zawadi hiyo ni sehemu ya utaratibu waliokuwa wamejiwekea baada ya kugundua wanakutana na majirani zao wa Stars kwani ilikuwa ni mechi yenye ushindani wa aina yake.
Spoti Xtra ambalo liko jijini hapa na limekuwa kwenye kambi mbalimbali karibu kila siku, limebaini pia kwamba kabla ya kutua hapa Harambee walijazwa minoti.
Kila mchezaji wa timu hiyo alipewa Sh17Mil kabla ya kukwea pipa kuja hapa Cairo kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu yamekuwa na ushindani wa aina yake.
Kenya na Tanzania zote kwa muda mmoja zitakuwa kwenye viwanja tofauti kesho Jumatatu zikichanga karata zao za mwisho za hatua ya makundi kwenye michuano hiyo.
Tanzania watakuwa wanakamilisha ratiba kwa kucheza na Algeria kwani hawana tena nafasi ya kusonga mbele huku Kenya wakicheza na Senegal. Kama timu zote mbili za Afrika Mashariki zitapoteza kesho, Jumanne mchana zitakuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kenya Mmoja
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments