KUMEKUCHA...Bernard Membe Ampa za uso Mbunge Lusinde..Afunguka Kuhusu Kushambuliwa | ZamotoHabari.



Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Bernard Membe amemjibu mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji kuwa anamsubiria atekeleze maagizo aliyopewa ya kumshambulia.



Membe aliyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Lusinde safiri salama ili utekeleze maagizo uliyopewa ya kunishambulia. Niguse ninuke!



Jana Lusinde alisema amemuweka kiporo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje ya nchi, Bernard Membe, hivyo atakaporudi nchini China atamshughulikia kwani  anamjua vizuri na hana chochote.

Alisema atakapomaliza ziara yake nchini China na kurejea nchini atamshughulikia kwani anamjua vizuri.



“Kuna mtu mmoja anaitwa Bernard Membe namuona anavyohangaika hangaika leo nina safari ya kwenda China kwa ziara ya kikazi. Membe namuweka kiporo nikirudi nitashgulika naye kwa sababu namjua vizuri na hana chochote,” alisema mbunge
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini