Na Zainab Nyamka na Cuthbert Kajuna, Michuzi Blog
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonna Kamoli amewapongeza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA kwa huduma nzuri wanayoitoa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Ameyasema hayo alipotembelea banda la DAWASA ndani ya maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.
Bonna ameipongeza DAWASA kwa kuweza kupeleka huduma ya majisafi kwenye maeneo mengi hususani kwenye yale ambayo hayakuwa na mtandao wa maji kwani katika uchaguzi wa mwaka 2015 ilikuwa ni moja ya ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kufikisha maji kwenye maeneo yote nchini.
Amesema, Dawasa wamejitahidi kufikisha maji ndani ya Jimbo la Segerea ingawa changamoto sehemu nyingine maji bado hayapatikani.
Ameeleza, jitihada kubwa zilizofanywa na Dawasa ni kubadili miundo mbinu ya maji iliyokuwa chakavu na kufanikisha kupatikana kwa maji ndani ya Jimbo la Segerea na viunga vyake.
Mbali na hilo, Bonna ameutaka uongozi wa Dawasa kutoa elimu kwa wananchi namna ya matumizi ya maji hususani kwa wadada wa kazi au watoto wanaowaacha majumbani pia kujaribu kuweka matanki ya maji ili kufahamu matumizi halisi ya maji.
Mhandisi wa Uendeshaji na Matengenezo Mkoa wa Tabata DAWASA Mhandisi Gibson Baragula amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa kuona kazi inayofanywa ya kupeleka maji sehemu zote za Mkoa wa Dar es salaam.
Amesema kwa sasa wanatoa maji kutoka bomba la Kimara kwenda hadi Bonyokwa na matarajio ni kuwa na wateja 3000 ila tayari wameshawaunganishia wateja 1400 na wateja 300 wameshafanya maombi ya maunganisho mapya na hivi karibuni wataanza kuwaunganishia.
Dawasa wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam katika banda lao ndani ya maonesho ya ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Jimbo la Segerea (CCM) Bonna Kamoli akipata maelezo kutoka kwa Afisa Huduma kwa kwa wateja alipotembelea banda la Dawasa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea na kupongeza juhudi za Mamlaka za kusambaza huduma ya Maji kwenye maeneo mbalimbali Jimboni kwake.
Mbunge wa Jimbo la Segerea (CCM) Mhe Bonna Kamoli akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la Dawasa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea na kupongeza juhudi za Mamlaka za kusambaza huduma ya Maji kwenye maeneo mbalimbali Jimboni kwake.
Mbunge wa Jimbo la Segerea (CCM) Mheshimiwa Bonna Kamoli akipata maelezo kutoka kwa Afisa Huduma kwa kwa wateja alipotembelea banda la Dawasa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea na kupongeza juhudi za Mamlaka za kusambaza huduma ya Maji kwenye maeneo mbalimbali Jimboni kwake.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments