Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MBUNIFU Ernest Maranya kutoka Taasisi ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi nchini(VETA) ametoa ushauri kwa Serikali kuangalia namna ya kuwepo kwa miongozo kwa ajili ya wagunduzi kwani kwa sasa changamoto iliyopo hakuna muongozo.
Maranya ambaye yupo katika banda la VETA katika maonesho ya biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa ili kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wanaeleweka kisheria kuna kila sababu ya wadau wa elimu kuhakikisha inakuwa na muongozo kwa ajili ya wabunifu.
Katika maonesho hayo Maranya ambaye amekuwa akionesha kifaa alichobuni kinachotoa elimu ya anga amesema pia ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuharakisha elimu ya anga kwa kutumia mfumo aliobuni ili utumike katika shule zote na kuongeza anashukuru Rais Dk.John Magufuli kwani wanatambua na kwa kupitia wasaidizi wake amekuwa akipata ushirikiano.
Pamoja na mambo mengine amefafanua changamoto ambayo anakumbana nayo ni kutokuwepo kea muongozo kwa ajili ya wagunduzi na kwamba nakumbuka huko nyumba alitaka kuingia jeshini lakini alikosa nafasi kwasababu ya kukosekana kwa muongozo.
"Nakumbuka nilitaka kwenda jeshini lakini watu wa michezo aina mbalimbali wakipata nafasi lakini waliofika kwangu inabidi iundwe kamati ya kujadili wanafanyaje na sababu hakuna muongozo. Ushauri wangu umefikia wakati wa kuwa na muongozo kwa ajili wagunduzi,"amesema Maranya.
Akizungumzia zaidi kuhusu namna ambavyo amefanya ugunduzi,Maranya amesema kuwa anawashukuru sana VETA ambao ndio wanamlea na hata mambo yote ya ugunduzi anayofanya anayafanyia akiwa hapo hata mfumo wa anga ameugundua akiwa VETA.
"Nipo VETA na ukweli ni kwamba wamenichukua na sasa wananilea na kunisaidia katika kuhakikisha naendelea kufanya ugunduzi. Mbali na kubuni mfumo wa anga pia kuna mfumo ambao nimeshauchora unaohusu mashine itakayokuwa inajiendesha bila kutumia mafuta wala umeme bali itaitumia nguvu itokanayo na uzito,"amesema Maranya.
Wakati huo huo amesema anaiomba Serikali na wadau wa elimu nchini kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono katika kufanikisha ubunifu wake unafika maeneo yote nchini.
Amesema pamoja na kugundua mfumo huo na kukubalika lakini bado msukumo wa kuruhusu kuanza kutumia mashuleni bado ingawa anashukuru wadau wa elimu wamekuwa waliofika kwake kujifunza na kualikwa kwenye baadhi ya shule kuuelezea kwa wanafunzi.
Mgunduzi Ernest Maranya akifafanua jambo kuhusu kifaa alichogundua kinachotoa elimu ya mfumo wa anga akiwa kwenye banda la VETA katika maonesho ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam
Mgunduzi Erest Maranya akielezea mfumo wa sayari unavyofanya kazi angani
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la VETA wakimsikiliza mgunduzi Ernest Maranya wakati anaelezea kifaa akichobuni ambacho kinazungumzia elimu ya anga
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments