*Yawahamasisha Watanzania kutembelea katika banda lao kuelezwa umuhimu wa nishati ya Jotoardhi nchini
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
OFISA Mawasiliano wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania( TGDC) Augustino Kasale amefafanua kwa kina majukumu ya kampuni hiyo huku akitoa rai kwa Watanzania wanaofika kwenye Maonesho ya Biashara viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kufika kwenye banda lao.
Akizungumza na Michuzi Blog pamoja na Michuzi TV leo akiwa kwenye maonesho hayo Kasale amesema kuwa kampuni hiyo ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongoza maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania kamaa kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) .
"Kampuni hii inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 na ilianza rasmi shughuli zake Julai 2014 kwa jukumu na mamlaka ya kutafiti,kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi kuanzisha umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.
" Sababu za kuanzishwa kwanTGDC imetokana na miongo mingi nchi yetu kukabiliwa na upungufu wa uzalishaji wa umeme wa kutosha kutokana na sababu mbalimbali .
"Serikali imechukua hatua kadhaa za kutanzua tatizo la mgao wa umeme na baadhi ya hatua hizo ni ghali sana na zimeathiri mazingira .Hivyo ili kuepuka kujirudia kwa matatizo haya ndipo iliamuariwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme vya nishati jadidifu vikiwemo jua, upepo na jotoardhi,"amesema Kasale.
Akifafanua zaidi amesema dhamira ya Kampuni hiyo ni kutoa huduma za maendeleo ya nishati ya jotoardhi za uhakika na ufanisi ,kusaidia dira ya maendeleo ya Taifa ,kuongeza ajira mpya kwa Watanzania,kuongeza uelewa na njia mbalimbali za matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi na kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.
Wakati lengo kuu la kampuni hiyo ni kuzalisha megawati 200 ifikapo mwaka 2025 huku baadhi ha majukumu ya msingi ni kuhimiza maendeleo ya rasilimali za jotoardhi ikiwemo utafiti,uchunguzi juu ya ardhi,kuchimba na uhakiki wa awali.Pia kufanya uendelezaji wa rasilimali ya jotoardhi kufikia hatua ya upembuzi yakinifu.
Kasale akizungumzia kuhusu nishati ya jotoardhi amesema nishati hiyo inatokana na joto linalotoka kwenye mwamba wenye joto unaochemsha maji yaliyoingia ardhini .Ni nishati safi na endelevu .
Amesema pia nirasilimali inayojulikana kuwa nishati jadidifu kutokana na mfumo wa kutumika tena unaorudisha maji ardhini baada ya mvuke kugeuzwa kuwa maji na kupoozwa kwa desturi joto linalotoka chini ya ardhi kwa kawaida halina kikomo.
" Rasilimali ya nishati ya jotoardhi inaanzia kwenye ardhi isiyo ya kina kirefu hadi kwenye maji ya moto na miamba ya joto iliyoko kilometa chache chini ya uso wa ardhi ,na chini zaidi kwenye miamba iliyoyeyuka yenye joto kali inayoitwa Magma,"amefafanua Kasale.
Kuhusu maendeleo ua jotoardhi nchini Tanzania Kasale amesema kuwa kwa kuwa miongoni mwa nchi zilizoko kwenye mfumo wa bonde la Ufa la Afrika Mashariki ,Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za jotoardhi ambazo hazijaendelezwa na zimefanyiwa utafiti wa kiwango kidogo tu.
"Kulingana na makadirio ya kinadharia ,Tanzania imejaaliwa kuwa na zaidi ya 5000 za nishati za jotoardhi zinazosibiri kuendelezwa.Wakati uzalishaji umeme wa jotoardhi ni kwamba chini ya ardhi kunatarajiwa kubaki na joto zaidi kwa mabilioni ya miaka ijayo na hivyo kuhakikisha upatikanaji wa mtiririko wa joto usio na kikomo," amesema.
Pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa maendeleo duniani yanategemea kwa kiasi kikubwa nishati ya uhakika na kwamba vipo vyanzo mbalimbali ambavyo kwa miaka mingi vimekuwa tegemeo la uzalishaji wa nishati kwa ajili ya viwanda na matumizi mengine.
"Kutokana na ongezeko la uhitaji wa nishati ya uhakika duniani ili kuendesha shughuli za uzalishaji mali baadhi ya nchi mfano Kenya, Ethiopia, Iceland na Marekani zimepiga hatua katika uvunaji na utumiaji wa nishati ya jotoardhi .Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizopitiwa na bonde la Ufa na bonde hilo lina viashiria vingi vinavyoonesha uwepo wa hifadhi ya rasilimali kubwa ya nishati jotoardhi ambayo inaweza kutumika kuzalisha umeme na matumizi mengine moja kwa moja," ameongeza.
Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi kufika kwenye banda lao ambalo lipo katika banda la TANESCO kwenye maonesho ya biashara kupata ufafanuzi kuhusu nishatii ya jotoardhi na faida zake kwa nchi.
Ofisa Mawasiliano kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania Augustino Kasale akifafanua jambo wakati akitoa maelezo kuhusu kampuni hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuomba wananchi kufika kwenye banda llilipo kwenye Maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Banda la Kampuni ya Uendelelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika Maonesho ya 43 Kimataifa ya Bashiashara ya Dar es Salaam
Wageni waliotembelea banda la TGDC wakipata elimu ya nishati ya jotoardhi katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Bashiashara ya Dar es Salaam
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments