Mgombea ubunge wa CCM Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ndio pekee aliyerejesha fomu za kuwania nafasi hiyo kati ya wagombea 13 waliojitokeza.
Mtaturu amerejesha fomu hiyo leo Alhamisi Julai 18, 2019 kabla ya saa 10:00 jioni, muda ambao wagombea wote waliochukua fomu walitakiwa kuwa wamezirejesha.
Wagombea wengine waliochukua fomu ni Hamidu Hussein (ADA-Thadea), Tirubya Mwanga (UPDP), Ameni Npondia (CCK), Amina Ramadhan (DP) na Ayuni John (UDP).
Wengine ni Amina Mcheka (AAF), Maulid Mustafa (ADC), Selemani Ntandu (CUF), Feruzy Fenezyson (NRA), Abdallah Tumbo (UMD), Donald Mwanga (TLP) na Masalio Kyara (SAU).
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Ikungi, Thomas Mwailafu akizungumza na Mwananchi amesema hadi muda wa mwisho wa uchukuaji na urejeshaji fomu unamalizika, ni Mtaturu pekee ndio aliyerejesha fomu.
Uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Julai 31, 2019 kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Tundu Lissu aliyepoteza sifa za kuwa mbunge kutokana na kutojaza fomu za mali na madeni na utoro bungeni.
Tayari Mwailafu amebandika fomu ya Mtaturu katika mbao za matangazo wa ofisi ya halmashauri ya Ikungi ili kutoa fursa ya watoa pingamizi hadi kesho Ijumaa saa 10 jioni.
Mwailafu amesema kama hakutakuwa na pingamizi lolote atamkabidhi cheti cha ubunge wa jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na Lissu tangu mwaka 2010 hadi Juni 28, 2019.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments