RITA YAENDELEA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA MAONESHO SABASABA | ZamotoHabari.

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), inatoa huduma mbalimbali ikiwamo vyeti vya kuzaliwa katika Maonyesho 43 ya biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa RITA, Josephat Kimaro amesema mbali na kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa pia wakala utatoa ushauri wa kisheria bure kuhusu masuala ya kuandika wosia na mirathi.

“Pia tutapokea maoni, maswali, ushauri na mapendekezo kuhusu huduma za Wakala,” amesema.Kimaro amesema RITA imekuwa ikishiriki maonesho hayo kila mwaka ambapo amewaomba wananchi wakifika sabasaba watahudumiwa kwa bora kwa wakati. 
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya vyeti vya kuzaliwa katika banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa RITA, Josephat Kimaro (kushoto) akizungumza kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo vyeti vya kuzaliwa katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), wakiwaelekeza wananchi namna ya kujaza fom za cheti cha kuzaliwa leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini