WALEMAVU 300 MOROGORO WAPEWA VIFAA WEZESHI NA SHIVYAWATA.. | ZamotoHabari.

Chama cha watu wenye ulemavu nchini shivyawata kimegawa vifaa wezeshi zaidi ya 300 kwa walemavu kutoka wilaya 4 za mkoa wa Morogoro, lengo likiwa ni kuwaepusha dhidi ya changamoto zinazowakabili na kuwaepusha na utegemezi.

Katika makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo amesema wazazi na walezi wa watu wenye ulemavu waachane na tabia ya kuwaficha watu hao hasa katika nyanja ya elimu jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo yao binafsi huku pia akishukuru wadau waliojitokeza kusaidia ufanikishaji wa zoezi la kupatikana kwa vifaa hivyo ikiwemo shirika la sigara tanzania tcc na shirika la kimataifa la tumbaku kutoka japan jti...

Mwenyekiti wa shivyawata Taifa Ummy Nderiananga ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuonesha dhamira ya kujenga haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwani wameshuhudui wakipatiwa nyadhifa kubwa kama mawaziri jambo ambalo limeiweka serikali ya tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache zinazothamini mchango wa viongozi kutoka watu wenye ulemavu..

Mkurugenzi wa mauzo wa TCC Victor Mashobe  aliyemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo amesema wameshirikiana na shivyawata kutoa msaada huo kwani watu wenye ulemavu wanauhitaji mkubwa kwani watu hao wanastahili kuwezeshwa ili waweze kujikwamua kiuchumi..

ugawaji wa vifaa hivyo umehusisha watu wenye ulemavu kutoka wilaya za kilosa 101, mvomero 66, ifakara 77 na morogoro mjini 73.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro katikati Regina  Chonjo,Mkurugenzi wa mauzo wa TCC Victor Mashobe,Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Azizi Abood wa kwanza kulia pamoja na wadau mbalimbali wakimkabidhi muhitaji baiskeli.

 baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa watu wenye ulemavu mkoani morogor
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mh Regina Chonjo katika picha ya pamoja na baadhi ya watu wenye ulemavu na viongozi wengine mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini