MALCOM Ally Masoud Kipanya ni mtoto wa Sara Chande ambaye amelala kitandani kwa miaka 12 akisumbuliwa na tatizo la udhaifu wa misuli unaosababisha kushindwa kufanya kitu chochote katika maisha yake.
Pamoja na hayo yote Malcolm ni kijana mwenye mtazamo chanya katika maisha yake na fikra zake, kwani amekuwa akiamini kuwa kuacha kulalamika ndiyo mwanzo wa kuwa na furaha maishani.
Akiwa hajiwezi kitandani, bado ana ndoto ambazo anataka kuzitimiza katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wagonjwa wenzake na watu wenye ulemavu na kufungua taasisi ambayo itakuwa na msaada kwa wahitaji.
VIDEO:
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments