Mlema "Mimi ni Staa Mkubwa Bongo..Pesa Imenitembelea, Nalipa Baunsa Milioni" | ZamotoHabari.


MAMBO mazuri! Kama Staa wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela naye kwa sasa analindwa na baunsa ambapo anataja sababu za kufanya hivyo.Akistorisha na Shusha Pumzi, Mlela alisema kwa sasa ameamua kuweka ulinzi ambapo anaongozana na baunsa kila anapokwenda kwa kuwa maisha yake yamebadilika baada ya fedha kumtembelea.

“Mimi ni staa mkubwa sana hapa Bongo na hata nje ya nchi hivyo ni lazima niwe na baunsa, hata mastaa wa nje wanafanya hivi, isitoshe kwa sasa fedha imenitembelea, tofauti na zamani, namlipa mshahara wa shilingi laki tano mpaka milioni moja kwa mwezi, inategemeana na tumefanya kazi kwa kiasi gani,” alisema Mlela.

Mlela ameongeza orodha ya mastaa ambao wanaolindwa na mabaunsa kama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na Lungi Maulanga.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini